Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 09.05.2019:

Haki miliki ya picha Getty Images

Mshambulaiji wa Brazil Philippe Coutinho, 26, sio mchezaji wa Barcelona na atakuwa kiungo wa kwanza wa timu hiyo kufuatia kuondolewa kwa timu hiyo katika nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya na Liverpool.

Bodi ya klabu hiyo pia inakutakana kuamua kuhusu hatma ya mkufunzi wa klabu hiyo Ernesto Valverde. (ESPN)

Marufuku ya usajili wa wachezaji wapya Chelsea ni habari mbaya sana kwa uhamisho wa mshambuliaji wa klabu hiyo na Ubelgiji Eden Hazard kuelekea Real Madrid na inaweza kuathiri uhamisho wa mchezaji huyo Uhispania. (AS)

Juventus na kocha wake Massimiliano Allegri, 51, wanatarajiwa kuachana baada ya misimu mitano pamoja na mataji matano ya ligi alioshinda. Mkufunzi na mchezaji wa zamani wa Juve Antonio Conte amehusishwa kuchukua nafasi hiyo.. (La Stampa - in Italian)

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29. anataka kusalia katika klabu ya Real Madrid lakini hajapata kuungwa mkono na mkufunzi wa timu hiyo Zinedine Zidane. (Sky Sports)

Kutakuwa na kombe kama lile la ligi ya Uingereza katika uwanja wa Anfield katika siku ya mwisho ya msimu siku ya Jumapili , huku kombe asili likiwa katika uwanja wa Amex ambapo viongozi wa ligi Manchester City itakabiliana dhidi ya Brighton. (Times)

Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester City itamsaini mshambuliaji wa Benfica na Ureno Joao Felix, 19, iwapo itamuuza mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus 22 . (A Bola - in Portuguese)

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Bayern hawafurahii ukufunzi wa timu hiyo chini ya kocha Niko Kovac. (Bild - in German)

Winga wa Swansea Danile James 21 ananyatiwa na Newcastle huku mshambuliaji wa Uhispania Ayoze Perez, 25, akitathmini uhamisho wa dau kubwa kuelekea Itali. (Mirror)

Ajenti wa Alexis Sanchez ameanza mazungumzo na Inter Milan kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 raia wa Chile kuhamia katika klabu hiyo kutoka Manchester United. (Gazzetta dello Sport)

Kipa wa taifa la Czech Petr Cech, 36, alikubali kwamba kibarua chake katika klabu ya Arsenal kilikwisha miezi kadhaa iliopita. (Evening Standard)

Everton inakabiliwa na ushindani mkubwa kumfanya Andre Gomes kuondoka katika klabu ya Barcelona huku Arsenal ikijiunga na klabu ya Roma na Inter Milan katika kuisaka saini ya kiungo huyo wa kati wa Ureno, 25. (Sun)

Nahodha na beki wa klabu ya Ajax mwenye umri wa miaka 19 Matthijs de Ligt amekataa fursa ya kujiunga na Manchester United msimu huu .(Daily Mail)

TETESI ZA SOKA JUMATANO

Haki miliki ya picha Getty Images

Real Madrid inatarajiwa kuwasilisha ofa itakayovunja rekodi ya dunia ya £240m kwa mshambuliaji wa Paris St-Germain 20,na Ufaransa Kylian Mbappe. (France Football, via Sport)

Mpango wa Manchester United wa kumnunua winga Jadon Sancho kwa dau la £100m umekufa baada ya timu hiyo ya ligi ya Uingereza kushindwa kufuzu katika michuano ya vilabu bingwa . (Mail)

Hatahivyo, United watafufua hamu yao ya kumnunua beki wa Leicester na Uingereza mwenye umri wa miaka 26 Harry Maguire mwisho wa msimu huu. (ESPN)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 28, anafikiria kuwasilisha ombi la uhamisho ili kulazimisha uhamisho wa kuelekea Real Madrid. (AS - in Spanish)

Chelsea tayari imekataa maombi mawili kutoka Real Madrid ili kumsajili Hazard. (Mirror)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp kwa mara nyengine atajaribu kumsaini kiungo wa kati wa Uhispania Marco Asensio, 23, kutoka Real Madrid. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Haki miliki ya picha Getty Images

Barcelona italazimika kufanya kazi ya ziada iwapo wanataka kuingia mkataba na beki wa Ajax mwenye umri wa miaka 19 Matthijs de Ligt baada ya ajenti wa mchezaji huyo kuwasilisha mahitaji mapya ya mchezaji huyo. (ESPN)

Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Antonio Conte amepinga kujiunga na klabu ya Roma . (La Gazzetta dello Sport - in Italian)

Roma huenda badala yake ikampatia fursa mkufunzi wa sasa wa Chelsea ili kurudi nchini Itali mwisho wa msimu huu . (Telegraph)

Winga wa Uholanzi na Fulham Ryan Babel, 32, anatarajiwa kuelekea katika klabu ya Galatasaray nchini Uturuki kwa uhamisho wa bila malipo. (Sun)

Arsenal itamwajiri aliyekuwa mchezaji wake wa zamani Edu kuwa mkurugenzi mpya wa maswala ya kiufundi katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu. (Mail)

Kiungo wa kati wa Wales Gareth Bale, 29, pamoja na viungo wa kati wa Uhispania Marcos Llorente, 24, na Dani Ceballos, 22, wameambiwa hawatakikani katika klabu hiyo na mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane. (Marca - in Spanish)

Winga wa Uskochi Ryan Fraser, 25,anatarajiwa kusalia katika klabu ya Bournemouth msimu ujao licha ya Arsenal kutaka kumsaini. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Newcastle na Uingereza Isaac Hayden, 24, anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu baada ya kufeli kulazimisha uhamisho Agosti iliopita. (Telegraph)

PSV itamuuza winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 21, na yule wa mexico Hirving Lozano, 23, ambao wamehusishwa na uhamisho wa Arsenal, Man United na Liverpool . (De Telegraaf - in Dutch)

Haki miliki ya picha Reuters

Ombi la Manchester United la kumsajili mchezaji wa Atletico Madrid Diego Godin lilijiri mwaka mmoja mapema kulingana na beki huyo wa Uruguay , ambaye ametangaza kuondoka katika klabu hiyo ya la liga mwisho wa msimu huu . (Manchester Evening News)

Godin, 33, amekubali kutia saini kandarasi ya miaka mitatu na timu ya Seria A Inter Milan. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Uhispania Juan Mata, 31, anataka kujiunga na Barcelona wakati kandarasi yake na Manchester United itakapokamilika mwisho wa msimu huu (Sport)

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE

Haki miliki ya picha Reuters

Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba, 26, anafikiria kuhamia Real Madrid mwisho wa msimu , lakini matumaini yake ya kuhamia klabu hiyo yatategemea Man United kupunguza thamani yake ya £160m. (Telegraph)

Pogba atalazimisha kuondoka hata iwapo Man United itakataa kumuuza. (ESPN)

Manchester City inakaribia kuingia makubaliano na kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, huku klabu hizo zikijadiliana kuhusu dau la kati ya £50m na £60m kwa mchezaji huyo wa Portugal mwenye umri wa miaka 24. (Sky Sports)

Matthijs de Lig Haki miliki ya picha Reuters

Beki wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, amekataa uhamisho wa kuelekea Manchester United wenye thamani ya £60m. (Star)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amejiunga katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Brazil na Ajax David Neres kwa dau la £35m . (Sun)

Manchester United iko tayari kuanza uhamisho wa wachezaji inaowalenga ili kuimarisha kikosi hicho na tayari imewasiliana na Juventus kuhusu kumsaini mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala kwa dau la £85m(Calciomercato, via Mail)

David Neres

Tottenham na Everton wanamuwania mshambuliaji wa Real Betis Giovani Lo Celso, 23. (Sun)

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, ameambiwa kwamba hatakikani katika klabu ya Real Madrid katika mkutano wa ana kwa ana na mkufunzi Zinedine Zidane, lakini bado anataka kusalia katika klabu hiyo . (Mail)

Mkufunzi wa Napoli na aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti ametoa ishara za kutaka kumsajili winga wa Mexico Hirving Lozano, 23, ambaye amehusishwa na uhamisho wa Manchester United. (Calciomercato)

Kieran Trippier

Ancelotti amekataa kupiga madai ya kutaka kumsajili beki wa Tottenham Kieran Trippier, 28, baada ya mke wa mchezaji huyo wa Uingereza kuonekana akitafutia shule watoto wake mjini Napoli.. (Talksport)

Winga wa Ufaransa Anthony Martial, 23, anakabiliwa na changamoto ya kumshawishi mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer kwamba ana kandarasi ya muda mrefu katika klabu hiyo.. (Mail)

Solskjaer atasikiliza kuhusu ofa za Martial zitakazowasilishwa kutokana na tabia yake mbaya wakati wa mazoezi.. (Sun)

Maajenti wa Martial wameandika katika mtandao wa instagram ili kutetea rekodi ya mshambuliaji huyo wa Man United huku kukiwa na ukosoaji kuhusu kiwango cha mchezo wa uwanjani Old Trafford.(Manchester Evening News)

Arsene Wenger

Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger, 69, amekataa ofa nyegine ya pili kuifunza klabu ya Fulham, baada ya kukataa kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Novemba kabla ya kumuajiri Claudio Ranieri.. (Mail)

Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Antonio Conte anasema kuwa kuna asilimia 60 kwamba huenda akarudi kufunza katika ligi ya Serie A msimu ujao.. (Le Iene - in Italian)

Newcastle United imekuwa ikimchunguza kiungo wa kati wa Uingereza na Coventry Tom Bayliss, 20, kabla ya kumsajili mwisho wa msimu huu . (Chronicle)

Kipa wa Poland Marcin Bulka, 19, anatarajiwa kuondoka Chelsea mwisho wa msimu huu na atatia saini kandarasi ya mapema na Paris Saint-Germain. (Goal.com)

Beki wa zamani wa Uingereza Gary Cahill, 33, ambaye anaondoka Chelsea mwisho wa msimu huu , anasema hajaridhika na soka ya kiwango cha juu na anasisitiza anaweza kuendelea kucheza. (Talksport)

TETESI ZA SOKA JUMATATU

tetesi

Tottenham inajiandaa kucheza msimu ujao bila ya kiungo wa kimataifa wa Denmark kiungo Christian Eriksen, 27, na wanaelekea kumsajili kiungo wa Ajax Donny Van de Beek 22, ambaye pia anatakiwa na Real Madrid na Bayern Munich.(Mirror )

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri ameitaka klabu yake kumsajili moja kwa moja mshambuliaji Gonzalo Higuain ambaye anaichezea Chelsea kwa mkopo akitokea Juventus ili kuimarisha kikosi chake. (Goal.com)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa kimataifa wa England Danny Welbeck, 28

Mchezaji wa kimataifa wa England Danny Welbeck, 28 hatopewa mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal na ataondoka akiwa mchezaji huru katika dirisha lijalo. (Sky Sports)

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane atamruhusu kiungo Luka Madric kuondoka. (AS)

Mchezaji wa kimataifa wa Venezuela Salomon Rondon, 29 ambaye anachezea Newcastle kwa mkopo amewaambia Magpies kutoangalia umri wake na kumnunua kwa sababu anafanana na mvinyo.(Mirror)

Winga wa Nice, Allan Saint-Maximin, 22, anayewaniwa na Arsenal na amefungua njia ya kujiunga na AC milan baada ya nafasi ya kujiunga na klabu hiyo mwezi januari kushindikana.

Image caption Tony Mowbray

Meneja wa Blackburn Tony Mowbray amejiweka mbali na ripoti zinazozungumzwa kuhusu klabu yake kutaka kumsajili goli kipa wa zamani wa England Joe Hart, 32.

Mlinzi wa Chelsea Kurt Zouma ambaye anacheza kwa mkopo katika timu y a Everton anatarajiwa kurejea Stamford Bridge kuanza maandalizi ya msimu mpya ingawa The toffees wanataka kumsajili kwa mkataba wa kudumu .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gary Cahill, 33

Nahodha wa Chelsea Gary Cahill, 33 na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England amemshambulia meneja wake Maurizio Sarri kwa kusema ameshindwa kumuonyesha heshima mchezaji huyo mkongwe wa Chelsea.

Klabu wa Celtic imetoa ofa kwa meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho, 56 kwa kumpa nafasi ya kuwa meneja wa klabu hiyo msimu ujao. (Sky Sports Italia, via Express)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii