Tanzania yavunja mkataba wa kuiuzia korosho kampuni ya Kenya

korosho Haki miliki ya picha Getty Images

Serikali ya Tanzania imesema mkataba wake na kampuni ya Kenya ya kununua korosho tani laki moja umesitishwa.

Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Joseph Kakunda , wakati akihojiwa na gazeti la Tanzania la "The CITIZEN" na kusema kuwa kampuni hiyo ya Indo Power wameshindwa kufuata masharti yaliyokuepo katika mkataba kwa wakati.

Mwezi Januari tarehe 30, serikali ya Tanzania kupitia Cereals na bodi nyingine ambazo ni ndogo zilizosainiwa na kampuni zinazofahamika chini ya kampuni hiyo ambayo ilikuwa kununua tani 100,000 za korosho ambazo zina thamani ya dola milioni 180.2.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Indo Power, Brian Mutembei alisema kuwa wakati wa kusaini mkataba hiyo ilikuwa ilipe moja kwa moja kupitia benki ya Tanzania kwa ajili ya kulipia korosho, na kuongeza kuwa biashara hiyo ingeanza mapema mwezi Februari.

Waziri Kakunda alisema kuwa licha ya kuwa kampuni ilishindwa kumalizia hatua muhimu za kisheria za mkataba huo. Na kuongeza kuwa serikali ilisaini mkataba na viwanda vingine sita ambao wanaweza kununua korosho hizo.

"Inabidi tusahau kuwa kampuni hiyo ilisaini mkataba na sisi huko Arusha(Indo Powe) kwa sababu imeshindwa kukidhi masharti ya makubaliano ambayo tulikubaliana nayo. Tumesaini mikataba na viwanda vingine sita , ambayo sasa tuko kwenye mchakato wa kumaliza makubaliano ambayo tulikubaliana.Na wanapaswa kufanya malipo kwanza kabla ya kuchukua mizigo," alisema

Waziri Kakunda amekataa kutaja majina ya makampuni hayo ingawa makampuni mawili kati ya hayo yanamilikiwa na wazawa huku nuingine zikiwa zinamilikiwa na watu kutoka nje ya nchi hiyo.

Aidha ameainisha kuwa makampuni hayo sita tayari yamekidhi matakwa ya mkataba, tani zote 222,000 za korosho ambazo zilivunwa msimu uliopita tayari zimeuzwa.

"Wiki iliyopita wawakilishi wa makampuni hayo ya kigeni walitembelea Tanzania ili kukagua miundombinu kama barabara na miundombinu kabla ya kutoa majibu katika nchi zao. Ila kwa ujumla tu, walionekana kuridhika" alisema.

Kwenye upande wa uhakika wa ubora wa bidhaa, Kakunda alisema kuwa korosho zimehifadhiwa mahali salama katika ghala ili kuhakikisha kuwa korosho hizo zinaendelea kuwa katika hali nzuri.

Kulikuwa kuna wasiwasi kuwa kampuni hiyo ya Indo Power haina uwezo wa kufanya biashara hiyo ambapo baadhi ya wadau walisema kampuni hiyo ya Kenya ilikuwa kama dalali tu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii