Watoto wanaokuwa katika ‘vijiji bila mama’ Indonesia

Ely Susiawati with a photo of her mother
Image caption Ely Susiawati akionesha picha ya mama yake

Ulimwengu unapoadhimisha Siku ya mama duniani: Indonesia Mashariki kuna sehemu ambako karibu kila mama aliye na umri mdogo ameenda kufanya kazi nje ya nchi.

Waindonesia wanayaita maeneo hayo "vijiji bila mama". BBC imewatambelea watoto hao kuangazia maisha yao bila 'mama'

Ely Susiawati alikua na miaka 11 mama yake alipomuacha chini ya ulezi wa bibi yake.

Wazazi wake walikua wametengana na ili aweze kukimu maisha ya familia yake changa na mama yake mzazi, Martia, aliamua kwenda nchini Saudi Arabia kufanya kazi ya ndani.

BBC ilipokutana na Ely, alikuwa mwaka wake wa mwisho shuleni. Alisema kuwa maisha yake ya yalikua magumu baada ya mama yake kuondoka nchini- ni wazi mpaka sasa kutengana kwao kunamuumiza sana.

"Ninapowaona marafiki zangu na wakiwa na mama zao kukiwa na hafla yoyote shuleni najihisi vibaya sana. Natamani sana mama yangu arudi nyumbani," alisema.

"Sitaki mama yangu awe anakuja na kuondoka kila wakati. Nataka awe nyumbani ili awalee wadogo zangu."

Katika kijiji cha kina Ely-Wanasaba, kilichopo Lombok Mashariki - Inaaminiwa kuwa kufanya kazi nje ya nchi ni jambo la kawaida na kina mama walio na umri mdogo huchukua hatua hiyo ili kuwahahikikishia watoto wao maisha mazuri.

Wengi wa wanaume katika eneo hilo wanafanya kazi ya ukulima au kazi za umma na inasemekana kuwa kipato chao nikifogo sana ikilinganishwa na wanawake wanaofanya kazi za ndani katika mataifa ya uarabuni.

Kina mama huaachia jamaa au waume zao jukumu la malezi - na kila mmoja analea mtoto wa ndugu au jamaa.

Lakini ni hali ya kusikitisha sana kwa watoto wanaotengana na wazazi wao.

Mama yake Karimatul Adibia alimuacha akiwa na mwaka mmoja na hata hakumbuki ni lini waliishi pamoja.

Alikutana na mama yake kwa mara ya kwanza alipokamilisha masomo ya shule ya msingi

Kabla ya wakati huo Karimatul alidhani ya kuwa shangazi yake aliyemlea ndiye kama mama yake mzazi.

"Nilichanganyikiwa sana," Karimatul alisema.

"Nakumbaka mama yangu yangu alilia sana. akimuuliza shangazi yangu, 'Kwanini mwanangu hanitambui kama kama mama yake?'

Shangazi ya Karimatul alimjibu kuwa hawakua na picha yake, na kwamba Karimatul alikwa akimtambua kama mama, ndio sababu ni vigumu kumuelewesha vinginevyo.

"Nilijawa na hisia kubwa ya kumkosa, lakini pia nilikuwa na hasiira kwanini aliniacha nikiwa mchanga," Karimatul anasema.

Sasa ana miaka 13, na yeyey huwasiliana na mama yake kila usiku kupitia simu ya video na wanatumiana ujumbe mfupi kila mara lakini hilo bado halija muondolea upweke wa kuishi bila mama.

"Hata mama yangu anapokuja likizo nyumbani, Nataka kuishi na shangazi yangu. Yeye huniomba nikae nae lakini namwambia kuwa nitakuja baadae."

Image caption Karimatul na shangazi yake Baiq

Shangazi yake ,Baiq Nurjannah, amewalea watoto tisa katika mazingira kama hayo na mtoto wake wa kumzaa ni mmoja tu.

Wengine wote ni watoto wa ndugu zake ambao wanafanya kazi nje ya nchi.

"Naitwa mama mkubwa," anasema huku akicheka.

Sasa ana miaka 50, na anatabasamu kwa furaha na kumshukuru Mungu akisemaalhamdulillah, katika kila sentensi.

"Nawalea wote kama watoto wangu," anasema. "Wanaishi pamoja kama ndugu na wote ni wazima najaribu kadri ya uwezo wangu kuwasikiliza wote."

Wanawake walianza kusafiri ughaibuni kufanya kazi katika eneo hilo la Indonesia miaka ya 1980.

Bila ulinzi wa kisheria wanawake hao wanakabiliwa na tisho la kudhulumiwa. Kumekuwa na visa vya baadhi yao kusafirishwa nyumbani kwenye majeneza.

Wengine kupigwa, kuumizwa au kutelekezwa na waajiri wao na wengine kutumikishwa bila malipo na kurudishwa nyumbani.

Kina mama wengine hurejea nyumbani na na watoto zaidi ambao wamewazaa kutokana na mahusiano mengine ya hiari nje ya nchi.

Watoto hao wanafahamika kama anak oleh-oleh - yaani vito vya watoto.

Kwa kuwa wamechanganya damu watoto hao huonekana tofauti katika kijiji hicho

Fatimah mwenye umri wa miaka 18 anasema kuwa wakati mwingine anafurahia utaofauti unaomfanya kuonekana jinsi alivyo.

"Watu wakati mwingine hunitazama kwa mshangao. Najua niko tofauti na watu wengine.

Wengine wana sema, 'Oh unapendeza sana,kwasababu una damu ya kiarabu.' maneno hayo hunifurahisha,"anasema huku akicheka.

Lakini wanaharakati wa kutetea haki ya wahamiaji wanasema watoto hao ''hubaguliwa'' nyumbani na shuleni pia.

Fatimah hajawahi kukutana na baba yake mwenye asili ya kiarabu lakini alikua akimtumia mama yake pesa za matumizi ili aweze kumlea yeye na ndugu zake wengine.

Lakini kwa bahati mbaya alifariki na baada ya hapo maisha yalikua magumu na mama yake Fatimah alirudi tena Saudi Arabia kufanya kazi.

Fatimah anasema kwa masikitika makubwa huku machozi yakimtiririka: "Hata kama mama hakurudi kufanya kazi Saudi Arabia tungeliweza kuishi pamoja kwa furaha pesa sio kila kitu."

Kundi la kutetea haki ya watoto wa wahamiaji limeungana na wanawake waliyo na watoto kama Fatimah ambaye amezaliwa kutokana na baba mwenye asili ya kiarabu na wale ambao mama zao wanafanya kazi nje ya nchi katika kijiji hicho kuwapatia elimu (mbadala) baada ya shule.

Watoto hao wanapoingia katika kituo hicho cha aelimu ya kidini wakiwa wamejifunika hijab za kupendeza mmoja wa waalimu anawaorodhesha kulingana na mataifa asili ya wazazi wao. "Malaysia, Saudi Arabia, Singapore, huyu ni Mwarabu, huyu ni Mmalaysia," anasema.

Kituo hicho kipo katika nyumba ya Suprihati, ambaye alienda kufanya kazi Saudi Arabia wakati watoto wake wawili wa kiume walilikuwa wachanga.

Ilikuwa uamuzi mgumu lakini ilizaa matunda, anasema.

Image caption Suprihati

"Nilipitia kipindi kigumu lakini iligeuka kuwa baraka kwangu."

Aliweza kuweka akiba na kuwasomesha watoto wake shule na sasa wanaishi maisha mazuri. Sasa hivi hafanyi kazi kusaidia familia yake.

Lakini kwasababu anafahamu fika changamoto wanazopitia watoto waliachwa nyuma na mama zao ameanzisha kituo maalum kinachowawezesha kukabiliana na maisha.

"Kulelewa na na jamaa zako sio sawa na malezi ya mama. Upendo wamama ni tofauti kabuisa. Watoto kama hao huonekana wapweke, kwa kujitenga hali ambayo wakati mwingine huwafanya kutojiamini," anasema.

Baada ya shule wao huja hapa na kwa kweli kituo hiki kimeleta mabadiliko, anasema.

"Tunawasidia kufanya kazi ya ziada ya shule na tunaona kweli wanataka kusoma. Tunapaita shule maalum na sasa wanaelekea kufikia viwango vya watoto wengine shuleni."

Zaidi ya thuluthi mbili ya wafanyikazi wahamiji wa Indonesia ni women, na pesa wanazolipwa wao hutuma nyumbani ili kukiwezesha kizazi kijacho kufikia ndoto ambao hawakua na matumaini ya kufikia.

Ely Susiawati hajamuona mama yake kwa miiaka 9, lakini mshahara anolipwa mama yake umemwezesha kuwa mtu wa kwanza kujiunga na chuo kikuu katika familia yake.

Anasomea elimu ya kifedha katika Chuo kikuu cha Mataram, na anasema kuwa sasa aneelewa kwanini mama yake aliamua kufanya uamuzi mgumu wa kumuacha kwenda kufanya kazi nje ya nchi

Image caption Ely

"Kam hakuenda, singelikua hapa nikiendelea na elimu yangu ya juu. Ananiwezesha kwa kila jambo maishani. Najivunia sana mama yangu. Yeye ni mwanamke jasiri! Hakuna mwanamkke jasiri kumliko mama yangu."

Wao huwasiliana kila mara kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp au Facetime.

" Kila wakati namwabia mahali nilipo na kumuomba ruhusa kila ninapotaka kuwatembelea marafiki zangu. Hatukutani ana kwa ana lakini tunawasiliana muda wote. Mama anajua kila kitu kinachofanyika maishani mwangu."

Alimpigia mama yake simu kwa njia ya video akiwa katika msikiti wa chuo kikuu ili azungumze na BBC.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii