Ikulu yasema kutoonekana hadharani kwa rais Uhuru Kenyata hakumaanishi hajulikani aliko

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Wakenya wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kuuliza maswali kuhusu mahali aliko rais wao Uhuru Kenyatta.

Bw. Kenyatta aliondoka nchi humo Aprili 23 kukutana na mwenzake Xi Jinping nchini China na inasadikiwa kuwa alirejea nyumbani kimya kimya Mey 3. Kwa mujibu wa gazeti la The Standard.

Kutoonekana hadharani kwa rais Kenyatta kumezua gumzo katika mitandao ya kijamii, huku wanasiasa wakipeana sababu tofauti kwa nini wanadhani raia ameamua kuwa kimya.

Msemaji wa Ikulu Kanze Dena amewajibu wa Wakenya wanaomuulizia rais Uhuru Kenyatta kwamba kiongozi wa nchi yuko ofisini na kuongeza kuwa yuko kazini kila siku.

Akijibu baadhi ya Wakenya waliyoanzisha kampeini ya kumtafuta rais Kenyatta, Bi Dena alisema kutoonekana hadharani kwa rais hakumaanishi hajulikani aliko.

"Nashagaa kusikia kuwa watu wanasema hawajamuona rasi tangu arejee nchini kutoka China, wakati rais amefanya mkutano na wakuu wa hazina ya Global Fund na kumekuwana taaarifa kuhusiana na mkutano huo," alisema Bi Dena.

Hata hivyo kupitia hashtag ya #FindPresidentUhuru, wakenya katika mtando wa kijamii wa Twitter maarufu KOT walituma ujumbe wa kutaka kujua rais Kenyatta yuko wapi.

Gavana wa jimbo la Machakos lililopo nje kidogo ya mji mkuu wa Nairobi, Dr. Alfred Mutua alinukuliwa na vyombo vya habari akimtetea rais kwa kutoonekana hadharani kwa mda.

''Rais ni meneja mwenye shughuli nyingi kwa hiyo anahitaji mmda wa kufanya mikutano, kupokea taarifa muhimu za serikali na kushughulikia masuala ya uchumi wa nchi'' alisema Bw. Mutua.

Aliongeza kuwa anashangaa kusikia watu wakiulizia kwanini rais hajaonekana hadharani tangu arejee kutoka ziara ya China.

Baadhi yao walijaribu kuelezea kwanini rais hajaonekana hadharani kwa majuma mawili.

Wengine wanadai kuwa rais kwanza alifuta akaunti zake rasmi za mitandao ya kijamii na kisha akaelekea ziara ya China kutafuta mkopo. Hivyo ndivyo rais wetu alivyotoweka! Yuko wapi Uhuru Kenyatta? walimalizia kwa kuuliza sawali hilo.

@KelvinShaban aliomuomba "Ndugu yake Raila aangazie aliko rais Kenyatta

Maneno kama vile Hashtags, tweets, retweets na memes hutumiwa sana katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Watu wengi walio na miaka zaidi ya 40 huenda wasiwa na ufahamu kuyahusu lakini maneno hayo huwaleta pamoja jamii ya wakenya inayofahamika kama KOT katika mtandao wa Twitter.

Hashtag zinazohusiana na masuala ya kisiasa sio maarufu kuliko masuala mengine ya kijamii, lakini hashtag ya #Kenya@50 ilitajwa kuwa miongoni mwa hashatag maarufu za kisiasa barani Afrika.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii