Imam wa miaka 100 'aliyehudhuria' ibada ya kanisa
Huwezi kusikiliza tena

Imam wa miaka 100 'aliyehudhuria' ibada ya kanisa

Imam mkuu wa Ghana ni mtu wa maneno machache lakini kiungozi huyo wa dini ya kidini mwenye umri wa miaka 100 ana uwezo wa kuwaleta watu pamoja.Picha za Sheikh Osman Sharubutu, akiwa ameketi katikati ya waumini wa Kikristo katika kanisa katoliki la Christ the King Catholic mjini Accra wakati wa ibada ya pasaka imezua gumzo katika mitandao ya kijamii. Je unadhani hatua kama hizi Zinaweza kuchangia utangamana wa watu bila kuzingatia misingi yao ya kidini? Tueleze kwenye ukurasa wetu wa facebook, bbcnewsSwahili.

Mada zinazohusiana