Mwanamume wa Kichina awekwa ndani kwa kuwapa mbwa majina yasiokubalika kisheria

Mbwa wa kichina mwenye jina lenye utata Haki miliki ya picha Beijing News
Image caption Jina la mbwa huyu lilimuweka matatani mmiliki wake

Mwanamume mmoja wa uchina amefungwa mashariki mwa Uchina kwa kuwapatia mbwa wake majina ''yasiyokubalika'' kisheria, imeripotiwa.

kwa mujibu wa gazeti maarufu nchini humo Beijing News, mmiliki wa mbwa mwenye umri wa miaka karibu 30 aliyetambulika kwa jina la kifamilia kama Ban anayeishi katika jimbo la mashraiki la Anhui Province aliitwa na polisi Jumatatu, baada ya kutuma picha ya mbwa wawili kupitia messenger WeChat kwa njia ya simu yake wakiwa na majina Chengguan na Xieguan

Majina hayo yaliibua utata kwasababu yalikuwa ni majina ya wafanyakazi wa huduma za serikali na kiraia wanaoheshimiwa.

"Chengguan" ni maafisa waliajiriwa katika maeneo ya mijini kukabiliana na uhalifu mdogo na "Xieguan" ni wafanyakazi wasio rasmi wa jamii kama vile wasaidizi wa maafisa wa usalama barabarani.

Gazeti hilo linasema Bwana Ban aliwapatia mbwa wake majina kwa ajli ya ''kujifurahisha'' lakini maafisa hawaoni mzaha wowote katika lolote.

Polisi wa Yingzhouwanasema wameanzisha uchunguzi mara moja juu ya mwanamume huyo, ambaye wanasema alikuwa ametoa taarifa za matusi dhidi ya wahudumu wa usalama.

Wameongeza kuwa, "kulingana na vipengele husika vya sheria ya wa watu wa Uchina kuhusu usalama wa umma ", lazima awekwe kwenye kituo cha mahabusu ya utawala iliyopo Xiangyang kwa siku 10.

Amesababisha madhara

Haki miliki ya picha Yingzhou Police
Image caption Bwana Ban lazima awekwe lumande kwa siku 10 kwa kuwaita mbwa wake majina yenye utata

Afisa wa polisi aliyetambuliwa kwa jina lake la ubini kama Li aliliambia gazeti la Beijing News kwamba Bwana Ban amekuwa akiendeleza uchokozi kwenye akaunti yake ya WeChat, na kuongeza kuwa hatua zake "zimesababisha madhara makubwa kwa taifa na kwa utawala wa jiji hasa upande wa hisia ".

Bwana Ban anasema anajutia matendo yake huku gazeti la Beijing New likimnukuu akisema "Sikujua sheria, sikujua hii ilikuwa ni kinyume cha sheria ."

Huku baadhi wakisema kuwa alikuwa ''anajitafutia matatizo ", kukamatwa kwake kumewashtua watumiaji wengi wa mtandao maarufu wa Sina Weibo microblog.

Watumiaji wengi wameonyesha hofu yao juu ya mazingira anamoshikiliwa Bwana Ban . "Unaweza kunieleza ni sheria gani inasema kuwa mbwa hawawezi kuitwa Chengguan?" mtumiaji mmoja wa blogi hiyo aliuuliza, na mwingine aliuliza : "Ni maneno gani mengine yanaweza kukufanya ufungwe?"

Baadhi ya watumiaji wamekuwa wakitania kuwa Bwana Ban ameshikiliwa kwasababu "kushukiwa kuupinga utawala wa taifa" au "kutoa siri za taifa", ikimaanisha kuwa, chengguan ni mbwa halisi.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Mbwa kutambua ugonjwa wa Malaria kwa kunusa

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii