Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 17.05.2019: Salah, Jovic, Griezmann, Alonso, Rashford, Aubameyang, Lacazette

Mo Salah Haki miliki ya picha Getty Images

Real Madrid inatarajiwa kujaribu tena kuwasilisha ombi kwa Liverpool msimu huu wa joto kumsajili mshambuliaji raia wa Misri Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 26. (Canal+, kupitia Mail)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Eintracht Frankfurt Luka Jovic, aliye na umri wa miaka 21, anakaribia kukamilisha uhamisho wa thamani ya £52.4m kwenda Real Madrid. (Sky Sports)

Barcelona inapanga kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 28, aliyetangaza mipango ya kutaka kuondoka Atletico Madrid. (Goal.com)

Manchester City ipo radhi kulipa kifungu kinachomfunga Griezmann katika mkataba wake. (Sport Witness, kupitia Manchester Evening News)

Mlinzi raia wa Uhispania wa Chelsea Marcos Alonso, mwenye umri wa miaka 28, anapigwa jicho na Atletico Madrid. (AS, kupitia Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Antoine Griezmann

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Manchester United Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21, na wachezaji wawili wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, aliye na miaka 29, na Alexandre Lacazette, wa miaka 27, ni wachezaji ambao wanaweza kulengwa na Barcelona. (Mundo Deportivo)

Mchezaji wa kiungo cha mbele raia wa Ujerumani anayeichezea Bayer Leverkusen Julian Brandt, mwenye umri wa miaka 23, huenda akazisusia timu mbili zilizo katika fainali za ubingwa wa Ulaya Tottenham na Liverpool ili kusalia Ujerumani. (Sky Germany, kupitia Mirror)

Matumaini ya mshambuliaji wa West Brom mwenye umri wa miaka 29 Salomon Rondon kupata uhamisho wa kudumu kwenda Newcastle kunategemea Rafa Benitez kusalia kuwa msimamizi huko St James' Park. (Newcastle Chronicle)

Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo anasema mchezaji anayelengwa na Manchester City Rodrigo, mchezaji wa kiungo cha mbele wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28 ataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto iwapo tu atataka mwenyewe kuondoka. (Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakuu wa Manchester United kumsaidia Ole Gunnar Solskjaer kuijenga upya klabu hiyo

Kaimu mwenyekiti mtendaji wa Manchester United Ed Woodward amekiri kutumia uzito wa fedha wa klabu hiyo kumsaidia Ole Gunnar Solskjaer kuijenga upya klabu hiyo baada ya msimu uliokuwa na 'mtikisiko'.(Sky Sports)

Ajenti wa mchezaji wa Atletico Madrid raia wa Ghana Thomas Partey, mwenye umri wa miaka 25, amebainisha dau la mchezaji huyo huku kukiwepo taarifa za Manchester United kutaka kumsajili. (Manchester Evening News)

Wolves inapanga uhamisho wa msimu wa joto wa mchezaji wa Reading mwenye umri wa miaka 18 Danny Loader. (Football Insider, kupitia Birmingham Mail)

Aliyekuwa mwenyekiti wa Crystal Palace Simon Jordan anaamini Eagles wanapswa kumuuza Wilfried Zaha msimu huu wa joto na anasema £60m ni thamani ya wastani kwa mchezaji huyo wa miaka 26 raia wa Ivory Coast. (Talksport)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Manchester United itafaidi £15m iwapo Crystal Palace itamuuza Zaha

Manchester United itafaidi £15m iwapo Crystal Palace itamuuza Zaha msimu huu wa joto kutokana na kifungu katika mkataba kuhusu kumuuza winga huyo wake wa zamani. (mail)

Bora za Alhamisi

Meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri mesema ataondoka Stamford Bridge hata akishinda ligi ya Europa- Roma na AC Milan huenda wakatafuta huduma za Mtaliano huyo, huku Blues wakitarajiwa kumsaka meneja wa Watford Javi Gracia. (Express)

Chelsea watatoa uamuzi kuhusu hatma ya Sarri kama kocha mkuu baada ya fainali ya ligi ya Europa ambapo watakipiga dhidi ya Arsenal Mei 29. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maurizio Sarri

Manchester United wanakaribia kumsajili winga wa kimataifa wa Wales na Swansea Daniel James, 21, licha ya tetesi kuwa huenda wakamkosa winga wa kimataifa wa England na Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19. (London Evening Standard)

Real Madrid watawaachilia hadi wachezaji 14 msimu huu wa joto, huku with mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Gareth Bale, 29, Kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 32, na mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia James Rodriguez, 27, wakitarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji hao. (Marca)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gareth Bale

Tottenham imesitisha mazungumzo ya uhamisho wa wachezaji wake wa timu ya kwanza hadi baada ya fainali ligi ya Mabingwa itakayochezwa June mosi. (London Evening Standard)

Hatahivyo Tottenham ni miongoni mwa vilabu vinavyofuatilia mchezo wa kiungo wa kati wa kimataifa wa Ujerumani na Bayer Leverkusen Julian Brandt, 23. (Mail)

Jose Mourinho anadai kuwa meneja akijifanya 'mtu mzuri ' huenda akageuka kuwa 'kikaragosi' katika ujumbe wake kwa meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer. (Talksport)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meneja wa zamani wa Manchester United ,Jose Mourinho

West Brom watafanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Brighton Chris Hughton wiki ijayo katika harakati za kumshawishi arejee katika usamamizi wa klabu hiyo. (Telegraph)

Barcelona wanaamini kuwa watamsajili kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28, kutoka Atletico Madrid msimu huu, licha ya kuwa Paris St-Germain pia wanamsaka nyota huyo .(London Evening Standard)

Griezmann hatachukua nafasi ya ya nyota wa zamani wa Liverpool Philippe Coutinho katika klabu ya Barcelona, kwa mujibu wa wa meneja wa mchezaji huyo raia wa Brazili. (Sky Sports)

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii