Allan Buberwa: Mwanafunzi wa kitanzania aliyefia mtoni Marekani azikwa Dar es salaam

Mwanafunzi aliyedumbukia mtoni Marekani kuzikwa Tanzania
Image caption Mwanafunzi aliyedumbukia mtoni Marekani azikwa Tanzania

Mwanafunzi wa Kitanzania aliyefariki Marekani wiki iliyopita, Allen Buberwa amezikwa leo baada ya mwili wake kurudishwa Tanzania jana Jumatano.

Buberwa alifariki baada ya kuteleza na kutumbukia kwenye mto Buffalo huko jimboni Arkansas, Marekani.

Buberwa na rafiki zake watatu walienda mtoni huku wawili kati yao wakiingia majini na kuogelea. Buberwa pamoja na kijana mwengine walisalia ukingoni mwa mto.

Ghafla Buberwa aliteleza na kutumbukia mtoni na kushindwa kujinasua, kijana mwenzie aliyekuwa naye pia alijirusha ili amuokoe lakini pia akanasa.

Rafiki zao wawili waliotangulia mtoni walijitahidi kuwaokoa lakini Buberwa alisalia chini ya maji.

Image caption Wazazi wake Allan Buberwa

"Familia kwa ujumla tunashukuru kwa kile ambacho kila mtu ambaye amejitoa kwa ajili ya mtoto wetu.

Watanzania ambao wanaishi nchini Marekani, ndugu , marafiki na jamaa walisaidia kutoa michango kwa kadri walivyoweza" imeeleza familia ya kijana Allen Buberwa, ambaye amefariki nchini Marekani mwanzoni mwa wiki.

Huku wanafunzi wenzake wanasema wataendelea kumsifu kwa jitihada zake katika masomo na hata jinsi alivyoweza kupata udhamini wa ada ya shule kwa jitihada zake mwenyewe.

Image caption Rafiki yake marehemu, Yasir Mohamed akiwa amebeba picha ya marehemu

Yasir Mohamed Simba ambaye ni rafiki yake marehemu Allen, anasema kuwa walikutana shuleni huko nchini Uganda wakati alipohamia darasa la nne mwaka 2006.

"Kitu kikubwa ambacho nitaendelea kukikumbuka kutoka kwa marehemu ni kuwa alikuwa anapenda sana michezo, ubishi ulikuwa mkubwa Manchester United inapocheza".

Huwezi kusikiliza tena
Allan Buberwa: Mwanafunzi wa kitanzania aliyefia mtoni Marekani azikwa Dar es salaam

"Lakini kikubwa ambacho siwezi kukisahau kutoka kwa marehemu Allen ni jinsi alivyokuwa ananisaidia kufanya homework kwa sababu alikuwa mwerevu zaidi darasani.

Vilevile alikuwa anajua lugha ya kiganda kwa sababu alikuwa amefika Uganda muda mrefu zaidi yetu hivyo alikuwa mwenyeji wetu na mara nyingine walimu walipokuwa wanachanganya lugha yao, yeye alikuwa anatusaidia kututafsiria" anasema Simba.

Mara ya mwisho marafiki hao wawili waliwasiliana siku tatu nyuma na mara nyingi anaongeza Simba na kwamba 'watu ambao tumesoma naye tumeumia sana na jana wakati tunapokea mwili ndio tumeamini kuwa hayuko na sisi tena".

Image caption Baba na mdogo wake Allan, Christina

"Alikuwa kaka na mzazi kwetu kwa sababu ndio alikuwa mkubwa kwetu wakati tunasoma Uganda.

Yeye ndio alikuwa kiongozi mzuri kwetu nyumbani na shuleni.

Alikuwa anapenda sana tambi, nakumbuka kuwa alikuwa anapenda kuchanganya sana parachichi kwenye chakula na kusikiliza muziki" mdogo wa Marehemu, Christina Buberwa.

Huku rafiki mwingine wa marehemu, Mash Francis Julius anasema kuwa aliwasiliana na rafiki yake ambaye aligeuka kuwa kaka yake.

Anasema kifo hicho kilimshtua sana kwa sababu muda mfupi tu kabla ya kupata taarifa ya kifo cha Allan, alikuwa anawasiliana naye kwa whatsapp.

Taarifa nyengine kuu

Kumbukumbu ya mwisho ambayo hawezi isahau ni picha ya pamoja ambayo marehemu mwenyewe alimuomba wapige wakati anaondoka.

Wasifu wa marehemu

Haki miliki ya picha FACEBOOK

Allen alizaliwa jijini Dar es Salaam, Tanzania Agosti 31, 1996.

Ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wanne ya Bw Audatus Rwegalulira na Bi Hilda Simon.

Ameacha wadogo zake watatu, mapacha Christina na Christabella, na wa mwisho Anatolius.

Alianza safari yake ya awali katika shule ya msingi St. Mary's na baadae kuhamishiwa nchini Uganda kwenye shule ya msingi ya Leons Junior hadi darasa la saba.

Aliendelea na masomo ya sekondari Uganda, kidato cha kwanza mpaka cha nne katika shule ya kidato cha kwanza mpaka cha nne St Henry 's College Kitovu na kidato cha tano na sita Shule ya Sekondari Masaka. Alimaliza safari yake ya elimu Uganda 2016.

"Baada ya hapo alianza harakati za kutafuta chuo, na alipenda sana kupata elimu ya kiwango cha juu sana na jambo jilo ndilo lililomsukuma kuelekea Marekani. Alitamani kufanyakazi kwenye sekta ya afya," amesema mjomba wa marehemu, Bw Simon.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii