Mwanafunzi wa Kitanzania aliyefia Marekani azikwa
Huwezi kusikiliza tena

Allan Buberwa: Mwanafunzi wa kitanzania aliyefia mtoni Marekani azikwa Dar es salaam

Mwanafunzi wa Kitanzania aliyefariki Marekani wiki iliyopita, Allen Buberwa amezikwa leo baada ya mwili wake kurudishwa Tanzania jana Jumatano.

Buberwa alifariki baada ya kuteleza na kutumbukia kwenye mto Buffalo huko jimboni Arkansas, Marekani.

Buberwa na rafiki zake watatu walienda mtoni huku wawili kati yao wakiingia majini na kuogelea. Buberwa pamoja na kijana mwengine walisalia ukingoni mwa mto.

Ghafla Buberwa aliteleza na kutumbukia mtoni na kushindwa kujinasua, kijana mwenzie aliyekuwa naye pia alijirusha ili amuokoe lakini pia akanasa.

Rafiki zao wawili waliotangulia mtoni walijitahidi kuwaokoa lakini Buberwa alisalia chini ya maji.