Mtandao wa kimataifa wa wizi wa pesa wavunjwa

Wajumbe wa ginge walitangaza ujuzi wao wa kuiba kupitia mitandao mbali mbali Haki miliki ya picha Image copyrightGETTY IMAGES

Genge la uhalifu wa kimataifa linalotumia mtandao kuiba dola milioni 100 kutoka kwa watu zaidi ya 40,000 limevunjwa.

Hii imefuatia operesheni kali ya polisi iliyofanyika katika mataifa ya Marekani , Bulgaria, Ujerumani , Georgia, Moldova na Ukraine.

Genge hilo liliweza kuiba kwa watumiaji wa kompyuta zenye programu ya software unaofahamika kama - GozNym malware- iliyotengenezwa kwa lengo la kuvuruga, kuhatribu au kuweza kuingia kwenye mfumo wa kompyuta bila idhini ya mtumiaji ambao ulinasa taarifa za huduma za benki za mtandao na hivyo kuweza kuingia kwenye akaunti za benki.

Genge hilo liliwajumuisha wahalifu ambao walitangaza ujuzi wao wa kuiba kupitia mitandao mbali mbali.

Taarifa juu ya harakati za kuvunja mtanao wa genge hilo zimetolewa katika makao makuu ya polisi ya shirikisho la polisi la Muungano wa Ulaya mjini The Hague Uholanzi.

Taarifa hiyo imesema kuwa uchunguzi uliowezesha kusambaratishwa kwa genge hilo haukuwa wa kawaida, hususan ushirikiano uliojitokeza baina ya maafisa wa polisi wa nchi mbali mbali.

Haki miliki ya picha Getty Images

Huduma ya uhalifu wa kimtandao:

Wajumbe 10 wa mtandao huo wa genge wamekwisha kushtakiwa katika mahakama ya Pittsburgh, nchini Marekani kwa makosa kadhaa , ukiwemo wizi wa pesa wa moja kwa moja kupitia mtandao na kuiba pesa hizo kwa kwa kutumia akaunti za benki za marekani na za nchi nyingine

Wajumbe watano wa genge hilo, raia wa urusi bado hawajapatikana , akiwemo mmoja aliyetengeneza programu ya wizi ya GozNym malware na kusimamia utendaji wake, akiuunganisha na mitandao mingine ya wahalifu wa kimtandao.

Wajumbe mbali mbali wengine wa genge hilo wanakaobiliwa na mashtaka ni pamoja na:

  • Kiongozi wa mtandao, pamoja na msaidizi wake wa masuala la kiufundi,wanaokabiliwa na mashtaka mjini Georgia.
  • Mjumbe mwingine , ambaye jukumu lake lilikuwa ni kuteka akaunti mbalimbali za benki , amesafirishwa kutoka Bulgaria hadi Marekani kukabiliana na mashataka.
  • Mjumbe wa henge aliyehifadhi data za programu ya GozNym malware kwa njia ya siri kuhakikisha hazionekani anakabiliwa na mashtaka mjini Moldova.
  • Wengine wawili wanakabiliwa na mashtakanchini Ujerumani ya wizi wa fedha.

Mwanasheria mkuu wa Western District of Pennsylvania, Scott Brady alisimama pamoja na waendesha mashtaka na maafisa wa kupambana na ugalifu wa kimtandao kutoka nchi tano nyingine ndani ya makao makuu yashirikisho la polisi la ulaya , kutangaza kuvunjwa kwa kile alichokitaja kama "njama za dunia".

Miongoni mwa waathiriwa wa wizi wa genge hilo ni wafanyabiashara wadogo, makampuni ya sheria, Ushirikiano wa kimataifa na mashirika mengine.

Moja ya mambo yaliyogunduliwa katika operesheni hiyo ni namna uuzaji wa ujuzi wa kimtandao ulivyokithiri, alisema Prof Alan Woodward, mwanasayansi wa kompyuta katika chuo kikuu cha Surrey.

" Watengenezaji wa hii malware walinadi 'huduma' yao ili wahalifu waweze kutumia huduma zao kutekeleza wizi katika benki.

"kile kinachofahamika kama 'uhalifu kama huduma' umekuwa ukiendelea kukua katika maika ya hivi karibuni na kuyawezesha magenge ya uhalifu kubadili mtindo wao wa wizi wa awali wa madawa ya kulevya na na kuanza uhalifu wa kimtandao." Anasema Prof Alan Woodward.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Uhalifu wa kimitandao unaweza kuangamizwa kwa njia gani Tanzania?

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii