Kampuni Boeing yatangaza kuboresha ndege yake ya 737 Max

Muundo na mfumo wa uongozaji wa ndege ya Boing 737 Max uliripotiwa kuwa chanzo cha ajali zake Haki miliki ya picha Getty Images

Boeing imeboresha mfumo wake ndege ya chapa -737 Max- iliyopigwa marufuku kufuatia ajali zilizosababisha vifo vya abiria wengi katika kipindi cha miezi mitano.

Kampuni hiyo ya Marekani imetangaza kuwa tayari imekwishafanya safari 270 za ndege ya 737 Max yenye programu iliyoboreshwa.

Imeongeza kuwa itatoa taarifa kwa utawala wa safari za anga nchini Marekani-Federal Aviation Administration (FAA) -juu ya namna rubani anavyowasiliana na waongozaji wa ndege na hatua anazopaswa kuchukua kwa matukio mbali mbali.

FAA inatarajia Boeing iwasilishe taarifa juu ya namna ilivyoboresha ndege yake kwa ajili ya kupewa idhini ya kupaa tena wiki ijayo.

Ndege ya Ethiopian Airlines ilianguka mwezi Machi na kuwauwa watu wote 157 waliokuwemo.

Haki miliki ya picha JONATHAN DRUION

Ajali hiyo ilifuatia mkasa wa Lion Air nchini Indonesia mwezi Octoba ambapo watu 189 walikufa.

Ajali zote mbili ziliihusika kasoro ya mfumo wa Boeing 737 Max -ambao ulikuwa ni mpya uliolenga kuboresha udhibiti wa ndege na kuizuiwia kuelekeza uso wake juu.

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES

Boeing ilisema kuwa mara taarifa juu ya namna marubani wanavyoonyeshwa jinsi ya kutumia mfumo ulioboreshwa itakapowasilishwa kwa FAA, itashirikiana na wafuatiliaji wa usalama wa ndege kufanya majaribio ya safari za ndege na kuwasilisha hati ya mwisho.

Mapema wiki hii FAA ilisema kuwa itafanya mkutano na waangalizi wa usalama wa safari za anga tarahe 23 Mei kutoka kote duniani kuwapatia taarifa za sasa juu ya tathmini ya mfumo ulioboreshwa wa Boeing na mafunzo mapya kwa marubani.

Unaweza pia kutizama:

Huwezi kusikiliza tena
Familia zaomboleza mkasa wa ajali ya ndege Ethiopia

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii