Kizza Besigye kuhusu muungano wa kisiasa na Bob Wine
Huwezi kusikiliza tena

Kizza Besigye asema ushirikiano wake na Bobi Wine ni sehemu ya mapambano

Mwezi Januari muswada wa kufuta kikomo cha umri wa miaka 75 ambao ulikuwa sheria Disemba 2017 ulihojiwa kwenye mahakama ya juu kabisa nchini Uganda.

Kupitisha sheria hiyo ilikuwa vuta nikuvute katika bunge la nchi hiyo kwani inamruhusu Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 74 fursa ya kuchaguliwa tena kama atapenda mwaka 2021.

Miongoni mwa wakosoaji wakuu wa sheria hii ni aliyekuwa kiongozi wa chama cha Forum for Democratic Change, FDC, Dr Kizza Besigye. Zuhura Yunus alizungumza na Dkt Besigye mwanzo akitaka kujua kama yupo tayari kushirikiana na mpinzani mwenzake Bobi Wine katika harakati za kisiasa.