Polisi walioharibu gari la Mbunge Bobi Wine kushtakiwa

Maafisa wa kikosi cha polisi cha kupambana na ghasia (FFU) walivunja madirisha ya gari la na baadae kuzuwia tamasha lake la Kyarenga Extra alilokuwa akienda kulifanya Haki miliki ya picha AFP

Maafisha wa polisi walioharibu gari la mbunge wa Upinzani Robert Kyagulanyi al maarufu Bobi Wine wakati alipotiwa nguvuni katika siku ya Jumatatu ya Pasaka watakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya nidhamu ya polisi ya matumizi ya nguvu kupita kiasi, amesema Msemaji wa polisi ya Uganda.

Maafisa wa kikosi cha polisi cha kupambana na ghasia (FFU) walivunja madirisha ya gari la Mbunge huyo wa Kyadondo mashariki kwenye barabara ya Busabala alipokuwa akielekea kwenye eneo la One Love Beach kwa ajili ya tamasha la muziki wake aliloliita Kyarenga Extra ambalo baadae lilizuiwa na maafisa wa usalama.

Maafisa walimzuwia mwanamuziki huyo aliyegeuka kuwa mwana siasa, na kupasua moja ya madirisha kabla ya kulipiga gesi ya kutoa machozi ndani na kumvuta nje ya gari.

Polisi walimrudisha hadi kwenye nyumba yake ya Magere, Kasangati katika wilaya ya Wakiso baada ya Inspekta mkuu wa polisi Okoth Ochola kupiga marufuku tamasha lake za muziki. Hivi karibuni, rais Museveni, katika taarifa yake, alilaani tukio hilo akisema kuwa polisi wangepaswa kuliburuza gari la mbunge huyo kokote ambako wangetaka kulipeleka.

" Pia sikubaliani na njia iliyotumiwa na polisi kupasua vioovya gari la Bobi Wine. Wangeburuza gari lake na kulipeleka kokote walikotaka kumpeleka ,"Alisema Bwana Museveni katika taarifa iliyotolewa tarehe 4 Mei, 2019.

Matokeo yake kitengo cha udhibiti wa viwango vya taaluma ya polisi (PSU) kinachunguza video zilizochukuliwa wakati wa tukio hilo ili kuwafikisha polisi mbele ya Mahakama ya Nidhamu ya polisi kujibu tuhuma za kutumia nguvu kupita kiasi.

Haki miliki ya picha AFP

Matumizi ya nguvu kupita kiasi ni kinyume cha sheria ya polisi nchini Uganda . Iwapo afisa wa polisi atapatikana na hatia hiyo hufutwa kazi au kupewa onyo kali.

Msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, anasema hawawezi kupuuza kauli ya rais kwasababu ndiye Mkuu wa Majeshi. Bwana Enanga anasema polisi watatumia utaratibu wa ndani ya polisi kwa kuzingatia maelezo ya rais na kuchukua uamuzi.

Hii si mara ya kwanza maafisa wa polisi kuharibu gari la mwanasiasa wa upinzani au kutumia nguvu kupita kiasi wakati wanapomkamata mwanasiasa

Si mara ya kwanza kwa wanasiasa wa upinzani uganda kushambuliwa

Wakati wa uchaguzi wa ubunge wa Arua MP Agosti mwaka jana , Bobi Wine akikamatwa kwa njia ya ukatili na kuteswa na maafisa wa jeshi la UPDF.

Haki miliki ya picha AFP

Dereva wake Yasin Kawuma alipigwa risasi na kuuawawa katika mchakato huo. Ingawa Bobi Wine alikwenda kupata matibabu nchini Marekani , hakuna afisa wa usalama aliyeshtakiwa kwa tukio hilo.

Wakati wa maadamano ya matembezi ya kuelekea kazini mwaka 2011- Walk to Work dhidi ya kupinga kupanda kwa garama za maisha nchini humo, Polisi waliharibu gari la kiongozi wa zamani wa chama cha FDC Dkt Kizza Besigye katika eneo la Mulago na kummwagia pilipili kwenye usoni .

Dkt Besigye alikimbizwa hospitalini na baadae kusafirishwa mjini Nairobi Kenya kwa ndege kwa ajili ya matibabu.

Je ushirikiano wa Bobi Wine na Besigye ni tisho kwa utawala wa Museveni?

Licha ya ukweli kwamba tukio hilo lililaaniwa ndani ya nchi na nje ya mipaka yake, hakuna afisa hata mmoja wa usalama aliyehusika aliyeadhibiwa hata baada ya picha ya video iliyoonyesha ukatili aliofanyiwa kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Kizza Besigye kuhusu muungano wa kisiasa na Bob Wine

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii