Prince William: Afunguka kuhusu kukabiliwa na msongo wa mawazo baada ya kifo cha mamake Bintimfalme Diana

Mwanamfalme Williams

Anasema kwamba alihisi uchungu ambao hajawahi kuusikia baada ya kifo cha mamake , Bintimfalme Diana. William alifichua hayo katika makala ya BBC kuhusu shinikizo ya kiakili.

Ametaka raia wa kawaida kuwalelewa na kuzungumzia kuhusu hisia zao kwa kuwa wao sio roboti.

Williams pia alizungumzia kuhusu vile urubani wa ambalensi ulivyomuacha kuhisi kana kwamba kifo kinakaribia.

Kifo cha Princess Diana

Anasema kwamba kukabiliana na kifo cha mamake - ambaye alifariki katika ajali ya barabarani 1997 -alihisi kwamba anaweza kuwaelewa wale ambao wamekuwa wakiwaomboleza wapendwa wao.

Anasema kwamba : Nimefikiria hili sana na najaribu kuelewa ni kwanini nahisi hivyo lakini nadhani unapofiliwa katika umri mdogo unaweza kukabiliana vyema na uchungu mkali unaokupata.

Nilihisi hivyo katika kazi chache nilizofanya , nilizielewa familia zilizofiliwa na kwamba nilikuwa naweza kukabiliana na tatizo hilo.

Alielezea tatizo la hisia la kuwa rubani wa ambalensi lilivyokuwa gumu hususana baada ya kutoka katika jeshi ambapo hisia huwekwa kando.

Haki miliki ya picha PA

Kazi ya Urubani

Alisema kuwa kazi ya kuwa rubani wa ambalensi ilikuwa ya wazi na alizungumzia kuhusu kukabiliana na hisia 'changa'. kila siku ambao uanakabiliana na familia ambao wanapokea habari mbaya ambazo wasingetarajia kuzipata siku baada ya siku.

''Hiyo hisia changa niliihisi ikijikusanya ndani yangu na nilihisi kwamba huenda ikaniathiri na kuwa tatizo kubwa'', niliamua kuizungumzia.

Katika makala hayo ya BBC1 yatakayoanza kupeperushwa hewani siku ya Jumapili , Williams anazungumza na mchezaji Peter Crouch na Danny Rose , wachezaji wa zamani Thierry Henry na Jermaine Jenas pamoja na mkufunzi wa Uingereza Gareth Southgate.

Wote walizungumzia kuhusu swala la shinikizo la kiakili ambalo wamekabiliana nalo katika maisha yao.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption A young Prince William with his mother Princess Diana in 1987

William na mamake na nduguye mwanamfalme Harry wamezungumzia kuhusu kifo cha mama yao wakati walipozindua kampeni ya afya ya kiakili kwa jina 'vichwa pamoja' kuweka wazi matatizo yao.

Familia hiyo ya kifalme mwezi uliopita iliungana kuzindua programu ya kutuma ujumbe katika simu miongoni mwa watu wanaokabiliwa na tatizo la kiakili.

William, Kate Meghan na Harry wameunga mkono kampeni hiyo kwa kutoa £3m katika wakfu wao.

Wakfu huo pia ulipokea £1.5m kutoka kwa kitengo cha BBC cha watoto masikini.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii