Arnold Schwarzenegger alipigwa teke katika hafla moja Afrika Kusini

Muigizaji wa marekani na gavana wa zamani wa jimbo la California Arnold Schwarzenegger (katikati ) Haki miliki ya picha AFP
Image caption Schwarzenegger aliwataka mashabiki wake kuangazia riadha badala ya shambulio hilo.

Kanda ya video imeonyesha kuwa nyota wa Hollywood Arnold Schwarzenegger akishambuliwa katika hafla moja nchini Afrika Kusini.

Gavana huyo wa zamani wa jimbo la California mwenye umri wa miaka 71 alikuwa akizungumza na mashabiki wake wakati wa mashindano ya kuruka kamba katika hafla yake ya michezo barani Afrika wakati mtu mmoja alipompiga teke kutoka nyuma.

Mshambuliaji huyo baadaye anaonekana akishikwa na kuzuiliwa baada ya kisa hicho.

Hatahivyo Schwarzenegger aliwashukuru mshabiki wake katika mtandao a Twitter wakiotaka kumjulia hali na kusisitia kuwa hakuna cha kujali.

Kanda hiyo ya Video iliosambazwa sana katika mitandao ya kijamii inamuonyesha Schwarzenegger akipiga picha na mashabiki wake katika mji wa Johannesburg katika hafla hiyo ya Jumamosi wakati mtu huyo alipomshambulia kwa teke kutoka nyuma yake.

Nyota huyo wa The Terminator anakaribia kuanguka baada ya teke hilo , huku mshambuliaji wake akianguka chini ambapo anakamatwa na walinzi.

Mtu huyo baadaye alikabidhiwa maafisa wa polisi Kulingana na maafisa wa hafla hiyo.

Baadaye Schwarzenegger alituma ujumbe wa Twitter kwa zaidi ya wafuasi wake milioni nne: Nilidhani nilisukumwa na kundi la watu , kitu kinachotokea mara kwa mara . niligundua kwamba nilipigwa teke wakati nilipoona kanda ya video kama mulivyoona.

Baadaye aliwashauri mashabiki wake kuangazia michezo iliokuwa ikiendelea badala ya shambulizi hilo.

Tuna michezo 90 hapa Afrika Kusini na wanamichezo 24,000 wa kila umri-kitu kinachotupatia moyo kushiriki.

Tuwaangazie wanariadha hawa, aliandika katika mtandao wake wa Twitter.

Hafla hiyo ya michezo ya Arnold Classic Afrika hufanyika kila mwezi Mei na hushirikisha michezo kadhaa ikiwemo ujengaji misuli na michezo ya kukabiliana .

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii