Vincent Kompany: Nitaifunza na kuichezea klabu ya Anderlecht Ubelgiji

Vincent kompany Haki miliki ya picha Getty Images

Vincent Kompany anasema kwamba hatua yake ya kujiunga na klabu ya Anderlecht kama mchezaji mkufunzi ni uamuzi mzuri na vilevile mgumu aliochukua baada ya kutangaza kwamba ameondoka Man City.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ametaka kandarasi ya miaka mitatu na klabu hiyo ya Ubelgiji baada ya kuhudumu kwa kipindi cha mika 11 patika klabu ya Etihad, miaka minane akiwa nahodha wa klabu hiyo.

Ushindi wa 6-0 katika kombe la FA dhidi ya Watford ilikuwa mechi ya mwisho ya Kompany, baada ya kushinda mataji manne ya ligi, natali mawili ya comb la FA pamoja na mataji manne ya kombe la ligi. Fatica barba ya wadi katika mtandao wake wa Facebook , beki huyo wa Ubelgiji alisema kwamba haamini kwamba anaondoka City.

"Mara kadhaa nimekuwa nikifikiria kuhusu siku hii , alisema. Mwisho umekuwa karibu kwa miaka mingi. Man City imenipatia kila kitu nami nimejaribu kujitolea kwa mali na hali."

Na katika barua ya pili iliotolewa saa chache baadaye , Kompany alitangaza hatua yake ya kuelekea katika klabu ya Anderlecht , amabo wamesema kuwa kuwasili kwake katika klabu hiyo kunaadhimisha 'kuwasili kwa mwanamfalme'.

"Nataka kugawana ujuzi wangu na kizazi kipya kijacho , alisema Kompany ambaye mara ya kwanza alijiunga na klabu ya Anderlecht akiwa na umri wa miaka sita.Kwa hilo nitawaingizia Ubelgiji ule uzalendo wa Manchester."

Ni wakati umefika kuondoka

Haki miliki ya picha Getty Images

Kompany alijiunga na City kutoka klabu ya Hamburg kama mlinzi wa kati mwaka 2008 na akatajwa kuwa nahodha wa klabu miaka mitatau baadaye.

Alifunga goli lake la mwisho dhidi ya Leicester City tarehe sita mwezi Mei, shuti kali kutoka miguu 25 ambalo lilipigiwa kura kama goli bora la msimu na kitengo cha BBC cha mechi ya siku.

Ushindi huo uliipandisha City juu kwa pointi moja katika kilele cha jedwali la ligi ya Uingereza kabla ya klabu hiyo kukamilisha msimu wao kwa ushindi dhidi ya klabu ya Brighton.

"Ni wakati umefika kwa mimi kuondoka," alisema Kompany, "Ijapokuwa ni vigumu kufanya hivyo , nawashukuru wale wote walionisaidia katika safari malum, na katika klabu maalum."

"Nakumbuka siku yangu ya kwanza kama ninavyoiona siku yangu ya mwisho. Nakumbuka ukarimu wa watu wa Manchester sitosahau vile mashabiki wa manchester City waliovyosalia kuniunga mkono kaaika waakt maya na kaaika waakt mzuri. Mbali na mengine mengi tuliyopitia , mumeniunga mkono na kunipatia motisha ya kutosalimu amri."

Mwenyekiti wa Man City

Mwenyekiti wa Man City Khaldoon al Mubarak alisema: "Kumekuwa na mchango mkubwa katika klabu ya manchester City lakini hakuna mchango kama ule uliotolewa na Kompany. Kwa muongo mmoja sasa amekuwa amekuwa maisha na damu ya klabu hii yenye talanta tele.

"Amekuwa sauti ya klabu hii katika chumba cha maandalizi na mtu mpole na balozi akiwa nje Kompany anajivunia klabu hii kama vile tulivyojivunia kuwa naye."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii