Arnold Schwarzenegger 'amesema kwamba hatomfungulia mashtaka mtu aliyemshambulia kwa teke nchini Afrika Kusini

Muigizaji wa marekani na gavana wa zamani wa jimbo la California Arnold Schwarzenegger (katikati) akiondoka katika hafla ya Arnold Classic Africa event Haki miliki ya picha AFP
Image caption Schwarzenegger aliwataka mashabiki wake kuangazia riadha badala ya shambulio hilo.

Nyota wa Hollywood Arnold Schwarzenegger amesema kuwa hatomfungulia mashtaka mtu aliyemshambulia katika hafla moja nchini Afrika Kusini.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 71 alikuwa akizungumza na mashabiki katika hafla yake ya Arnold Classic Africa sporting event iku ya Jumamosi wakati mtu alipomrukia na kumpiga teke mgongoni.

Mshambuliaji huyo baadaye alikamatwa na kuzuiwa. Hatahivyo siku ya Jumapili , Schwarzenegger alisema kwamba hatomchukulia hatua mtu aliyemshambulia akisema tukio hilo limepitwa na wakati.

Kanda hiyo ya video ,iliosamabazwa katika mitandao ya kijamii ilimuonyesha Schwarzenegger akipiga picha na mashabiki wake wakati mtu aliyemshambulia alipotoka nyuma na kupiga flying kick.

Nyota huyo wa filamu ya Terminator aliteteleka karibu aanguke huku mshambuliaji akianguka ardhini ambapo anakamatwa na walinzi mara moja.

Haki miliki ya picha AFP

Mtu huyo ambaye jina lake halikutajwa baadaye alikabidhiwa maafisa wa polisi, kulingana na maafisa wa hafla hiyo.

Schwarzenegger alituma ujumbe wa twitter kwa zaidi ya mashabiki wake milioni nne: Nilidhania kwamba nilikuwa nimesukumwa na watu waliojaa katika hafla hii , ambacho ni kitu cha kawaida.

Niligundua kwamba nilipigwa teke nilipoona kanda ya video kama vile nyinyi. Akijibu ujumbe wa twitter kutoka kwa mashabiki wake siku ya Jumapili, alisema kwamba hatomfungulia mashtaka mashambuliaji wake.

''Tuna michezo 90 hapa Afrika Kusini na wanamichezo 24,000 wa kila umri-kitu kinachotupatia moyo kushiriki.Tuwaangazie wanariadha hawa'', aliandika katika mtandao wake wa Twitter.

Hafla hiyo ya michezo ya Arnold Classic Afrika hufanyika kila mwezi Mei na hushirikisha michezo kadhaa ikiwemo ujengaji misuli na michezo ya kukabiliana

Mada zinazohusiana