Uchaguzi Malawi: Mauaji ya Albino na taarifa za uongo za kifo cha rais Mutharika na mengineyo muhimu

Three main candidates Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Peter Mutharika (kulia) inakabiliwa na upinzani kutoka kwa Lazarus Chakwera (kushoto) na Saulos Chilima (kati)

Takriban raia milioni 7 nchini Malawi watapata fursa ya kumpigia kura rais mpya kesho Jumanne Mei 21 katika uchaguzi ambao hauwezi kutabirika katika historia ya nchi hiyo.

1. Makamu wa rais asimama dhidi ya Rais

Maswali mengi kuhusu iwapo afya ya rais Peter Mutharika inamruhusu kugombea muhula mwingine umezusha mgawanyiko na makamu wake wa rais, Saulos Chilima.

Chilima aliteuliwa na rais Mutharika kama mgombea mwenza wake katika uchaguzi uliopita mnamo 2014. Lakini mwaka uliopita shemegi yake rais, Callista Mutharika, alipendekeza kwamba umri wa kiongozi huyo , miaka 78, ni mkubwa kwa yeye kuchagulia tena na kwamba sasa atoe fursa kwa makamu wake aliye na umri wa miaka 46.

Pendekezo hilo lilipingwa na wafuasi wenye ushawishi katika chama tawala cha Democratic Progressive Party (DPP).

Kulizuka mgawanyiko wa chama hicho pande mbili, na hatimaye Chilima aliishia kuanzisha chama cha UTM, huku akisalia kuwa makamu wa rais nchini.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Inadhaniwa makamu wa rais Saulos Chilima ana umaarufu mkubwa miongoni mwa wapiga kura vijana nchini

Haijulikani wazi iwapo Bi Mutharika wana sikizana na shemegi yake - hivi karibuni hakuhudhuria uzinduzi wa sanamu la marehemu mumewe Bingu wa Mutharika. Anagombea ubunge kupitia chama hicho cha makamu wa rais UTM.

Chilima anaonekana kama ishara ya mabadiliko kwa raia nchini Malawi wanaotamani mageuzi.

Umri mdogo wa Chilima huenda ukawa na manufaa kwake, wakati raia walio na umri wa katiya miaka 18 na 34 wakiwa wanajumlisha 54% ya wapiga kura nchini.

2. Mke wa makamu wa rais 'afoka' kumtafutia mumewe kura

Mkewe Chilima, Mary, ameingia uwanjani akitafuta ushindi wa vijana kwa kuanza kuimba nyimbo za kufoka foka au rap.

Katika kanda ya video, kando na kufoka, anadensi na kutumia mistari inayofahamika kwa vijana huku akionekana kuvaa nguo kama wao.

Amewasilisha pia matangazo ya biashara yanayowalenga wapiga kura wanawake.

Wagombea ni kina nani?

Wagombea saba wapo kwenye debe katika uchaguzi wa urais Malawi, lakini watatu ndio wanaopigiwa upatu kuwa na nafasi ya kushinda:

  • Peter Mutharika - Democratic Progressive Party - rais wa sasa anayegombea muhula wa pili
  • Lazarus Chakwera - Malawi Congress Party - Anatumai kufufua utajiri wa chama tawala cha zamani
  • Saulos Chilima - UTM Party - makamu wa rais hivi sasa anayewania kiti dhidi ya mku wake

3. Hakuna wagombea wanawake wa urais

Licha ya kwamba wanawake ni 56% ya wapiga kura nchini, hakuna mwanamke anayegombea urais nchini.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanawake ni zaidi ya nusu ya idadi ya wapiga kura nchini lakini hakuna mwanamke anayegombea katika uchaguzi mkuu

Rais wa zamani Joyce Banda, aliyeshndwa na Mutharika mnamo 2014, alijitoa katika kinyang'anyiro hicho kumuunga mkono Lazarus Chakwera wa chama cha Malawi Congress Party (MCP).

Uchaguzi wa ubunge na udiwani pia unafanyika kwa pamoja katika uchaguzi huuu. zaidi ya wanawake 300 wanagombea viti katika bunge la uwakilishi wa viti 153. Huku mamia wengine wakigombea katika viti vya serikali za mitaa.

'Chanjo ya kwanza ya malaria' kufanyiwa majaribio

Tanzania yawasaidia waathiriwa wa Kimbunga Idai

‘Anusurika kunyongwa mara tatu’

4. 'Sijakufa' asema Rais Mutharika

Takriban wiki moja ikiwa imesalia kwa uchaguzi mkuu kufanyika, kumekuwa na uvumi uliosambaa kwamba rais Mutharika huenda ni mgonjwa mahututi au amefariki. Hili lilifuatwa kwa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ofisini mwake iliosema kwamba anakatiza mikutano mingine ya kampeni ili "kushughulikia mambo mengine muhimu zaidi".

Picha ya ndege ya ambulensi ya Afrika kusini, iliyokuwa katika uwanja mkuu wandege wa nchi hiyo, ilianza kusamba aktika mitandao ya kijamii iliyoongeza chumvi uvumi huo.

Mutharika alizuka upya katika kampeni siku mbili baadaye na kuwakejeli upinzani.

Alisema kwamba badala ya yeye kufa, ni wapinzani ake watakaoteseka kwa kifo cha kisiasa uchaguzi utakapofika.

"Je nimekaa kama maiti kwenu?" aliwauliza wafuasi wake.

Kumeshuhudiwa ghasia kwa kiasi fulani lakini kwa ukubwa kampeni zimekuwa za amani.

Hakuna duru ya pili ya uchaguzi katika uchaguzi huo wa rais Malawi - mgombea atakayejinyakulia kura nyingi ndiye mshindi.

5. Mauaji ya walemavu wa ngozi - Albino

Suala jingine lililogubika kampeni nchin ini mfululizo wa mauajai ya watu wenye ulemavu wa ngozi - Albino- kufuatia kuwadia kwa uchaguzi mkuu.

Kuna wasiwasi kwamba huenda suala hilo likaharabu nafasi ya makamu wa rais.

Ripoti ya Umoja wa matiafa imeashiria kwamba mashambulio na mauaji ya walemavu wa ngozi huongezeka wakati wa uchaguzi "kutokanana imani potofu kwamba viungo vya walemavu vinaweza kuleta bahati nzuri na nguvu za kisiasa na hutumika katika visa vya uchawi".

Vyama vya upinzan vinautuhumu utawala wa Mutharika kwa kutowajibika ipasavyo kusitisha mashambulio hayo.

Rais analikana hilo na ameunda tume ya uchunguzi, kuchunguza mauaji hayo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea