Huawei kutotumia Android: Afrika inaathirika namna gani?

Huawei

Chanzo cha picha, Getty Images

Bara la Afrika kuna takriban watu milioni 400 wanaotumia mtandao na kati ya hao kuna 60% wanatumia mfumo wa Android ambao ndio unatumikwa kwa simu kama za Huawei.

Ikiwa na soko lenye ukubwa wa takribani asilimia kumi na sita duniani, kampuni hiyo inatajwa kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa kubwa zaidi ya utengenezaji simu.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na hofu kutoka baadhi ya wadadisi kwamba huenda kampuni hiyo inatumiwa na Uchina kufanyia serikali za nje na pia wananchi wake ujasusi.

Lakini barani Afrika, kampuni hiyo pamoja na ile ya ZTE zimehusika sana katika ujenzi wa miundo mbinu nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, miongoni mwa mataifa mengine.

Nchini Nigeria kwa mfano, Huawei ilishinda kandarasi ya dola milioni themanini kutengeneza mtandao wa dijitali wa simu wa GSM mnamo mwaka 2004.

Kwa kutathmini ukubwa wa uwepo wa kampuni hiyo Afrika wadadisi wanasema mzozo unaoshuhudiwa sasa inamaanisha kwamba biashara nyingi zitaathirika kutokana na changamoto ambazo Huawei inakumbana nazo.

Barrack Otieno ambaye ni mtaalamu wa maswala ya sera za mtandaoni anaeleza kwamba, 'Waafrika wengi wanapokea mikopo midogo kupitia programu tumishi za simu ambazo zinatumia mfumo huo wa Android. Huenda sasa ikachangia watu wengi wakakosa mikopo na hivyo kuumia sana katika sekta za kibiashara'.

Huawei pia imezindua zaidi ya mitandao hamsini ya 3G, na kutengeneza mitandao ya huduma za zaidi ya serikali thelathini. Aidha kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika teknolojia zinazokua za 4G na 5G.

Mauzo ya Huawei yamekuwa katika kila bara . Mapato ni ya mabilioni ya dola za Marekani.  EMEA: Afrika mashariki, Ulaya, Mashariki ya kati .

Je kuna namna ya kuiepuka athari?

Wananchi wengi hununua simu za Huawei kwasababau ni za bei nafuu katika masoko ya simu Afrika.

Wanauchumi wanaonya ikiwa simu hizo sasa zitaondolewa katika soko kutokana na athari ya yanayoshuhudiwa, ina maana itaathiri pia uchumi wa kieneo, na zaidi 'nchi ambazo hazina nguvu kiuchumi'.

Serikali nyingi Afrika zinatumia teknolojia na miundo mbinu ya Huawei. Je zinapaswa kuwa na wasiwasi?

Barrack Otieno anasema huenda biashara nyingi zikasambaratika kwasababu biashara nyingi zimeundwa kwa msingi wa biashara ya Huawei.

'Kusema kwamba biashara hizo zibadilishwe kwa muda mfupi kama inavyopendekeza Marekani itakuwa sio jambo la rahisi' anaeleza.

Mchambuzi wa masuala ya intaneti barrack Otieno.
BBC
Waafrika wengi wanapokea mikopo midogo kupitia app za simu ambazo zinatumia mfumo wa Android. Huenda ikachangia wengi sasa kukosa mikopo na hivyo kuathiri biashara"
Barrack Otieno
Mtaalamu wa sera za mtandao

Marufuku iliyoidhinishwa kwa Huawei kutotumia mfumo wa Android unagubika uzinduzi hii leo kwa simu mpya za kampuni hiyo ya China.

Huawei imealikwa waandishi wa habari wa kimataifa kushuhudia uzinduzi wa simu mpya za Honor 20 Series.

BBC inafahamu kwamba simu hizo zitakuwa na uwezo wa kutumia kikamilifu Android.

Mwaka jana, Huawei iliunda simu milioni mia mbili na nane, huku nusu ya simu hizo zikiuzwa nje ya Uchina.

Huawei inaunda simu zaidi kushinda Apple. Hisa ya soko ya kampuni za kutengeneza simu (%).  .

Julai mwaka huo huo, kampuni hiyo iliipiku mshindani wake Apple na kuchukua nafasi ya pili katika utengenezaji simu janja duniani, huku Samsung ikisalia kileleni.

Lakini mpaka pale tofuai za kibiashara na Marekani zitakapotatuliwa, huenda simu zitakazo zinduliwa katika miaka ijayo zikawa na manufaa kidogo - iwapo hazitotumia mfumo huo wa Android.

Na pia haijulikani wazi iwapo marufuku ya Google kwa Android ni ya muda mrefu.