Pakistan: Watoto waambukizwa virusi vya HIV katika mazingira ya kutatanisha

Daktari mmoja amekamatwa nchini Pakistan kufuatia mlipuko huo wa ugonjwa ambao umeathiri watoto zaidi katika mazingira yenye utata Haki miliki ya picha AFP
Image caption Daktari mmoja amekamatwa nchini Pakistan kufuatia mlipuko huo wa HIV ambao umeathiri watoto zaidi katika mazingira yenye utata

Dalili ya kwanza kuashiria kwamba kulikua na tatizo katika kijiji cha Ratto Dero kusini mwa Pakistani ilijitokeza mwezi Februari.

Wazazi kadhaa walikua wamewapeleka watoto wao hospitali wakilalamika kuwa wanapatikana homa ya mara kwa mara.

Katika kipindi cha majuma kadhaa wazazi wengine walijitokeza na watoto wao wakiwa na dalili sawa na hizo.

Ili kubaini tatizo liko wapi, Dr Imran Aarbani aliagiza watoto hao wafanyiwe uchunguzi wa kina wa kimatibabu.

Matokeo ya uchunguzi huo ulithibitisha kuwa wameambukizwa virusi vya HIV - na hakuna anayejua ilikuaje.

"Kufikia Aprili 24, watoto 15 waligunduliwa kuwa na virusi vya HIV, japo wazazi wao hawakuwa na virusi hivyo," Daktari wa hospitali hiyo aliimbia BBC.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya watu wanafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika maeneo tofauti nchini humo

Kutoka wakati huo zaidi ya watu 607 -wengi wao watoto (75%) - wamepatikana na virusi vya HIV baada ya fununu ya mlipuko wa ugonjwa huo kuzifanya familia kadhaa kufika katika kambi maalum iliyoazishwa na hospitali ya serikali katika mji huo uliyopo mkoa wa Sindh.

Cha kushangaza ni kuwa huu si mlipuko wa kwanza kukumba eneo hilo japo huu wa sasa umekuja miaka kadhaa baadae.

Mlipuko kama huo wa virusi vya HIV ulishuhudiwa mwaka 2016 ambapo maelfu ya watu katika kijiji cha Ratto Dero walifanyiwa vipimo.

Wakati huo watu 1,521 walipatikana na virusi hivyo, kwa mujibu wa data zilizopo za mpango wa kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi mkoani Sindh (SACP).

Idadi kubwa ya watu waliyokua na virusi hivyo walikua wanaume na maambukizi hayo yalihusishwa biashara ya ngono ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Wakati huo msako mkali ulifanywa dhidi ya makundi hayo ya watu na japo ukahaba umepigwa marufuku biashara hiyo imeendelea kupata umaarufu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Utumiaji wa sindano moja kwa watu wengi unashukiwa kuwa chanzo cha mlipuko wa maabukizi mapya japo uchunguzi bado unaendelea

Lakini maambukizi haya ya sasa yanawza kahusishwa na maafisa wa afya?

Dr Asad Memon, ambaye ni mshirikishi mkuu wa SACP mjini Larkana, anaamini hilo linawezekana- japo sio moja kwa moja.

"Nadhani virusi vya (Ukimwi) kutoka kwa makundi hatarishi kama vile (wapenzi wa jinsia moja na wanawake wanaofanya biashara ya ngono) viliambukizwa wagonjwa wengine kupitia wahudumu bandia wa afya," aliiambia BBC.

Katika maeneo hasa ya vijijini nchini Pakistan, watu hutafuta huduma za afya kutoka kwa wahudumu "bandia" wa afya badala ya kumuona daktari aliyehitimu kwasababu inasadikiwa kuwa huduma yao ni bei nafuu,inapatikana kiurahisi,na pia huchukua muda kuwaelewa wagonjwa wao .

Dr Fatima Mir,ambaye anafanya kazi katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan anaamini utepetevu katika sekta ya afya ulichengia mlipuko wa mwaka 2016.

"Kuna njia tatu tu ambayo mtoto anaweza kuambukizwa virusi," anaelezea. "Huenda ikawa kupitia maziwa ya mama anayenyonyesha akiwa na virusi hivyo, kupitia utoaji wa damu, au kupitia vifaa vya matibabu kama vile sindano."

Katika visa vingi wazazi wa watoto aliyotangamana nao walifanyiwa vipimo na hawakua na virusi vya HIV, kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa wagonjwa kadhaa walitibiwa katika kliniki ya vijijini kwa kutumia sindano moja

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dr Muzaffar Ghangro alikamatwa kwa kushukiwa kuwa anaeneza maambukizi ya Ukimwi kwa kutumia sindano moja kuhudumia wagonjwa kadhaa katika kliniki yake- madai ambayo amekanusha

Maafisa pia wanaonekana kukubaliana na wazo hilo.

Karibu kliniki 500 ambazo hazitaimiza masharti yaliyowekwa zimefungwa kote mkoani humo, kwa mujibu wa mamlaka ya afya.

Mtaalamu wa masuala ya watoto, Dr Muzaffar Ghangro, pia amekamatwa na kushitakiwa kwa tuhuma za kueneza maambukizi ya virusi vya HIV kwa kutumia sindano moja kuhudumia wagonjwa kadhaa.

Amekanusha madai hayo akijitetea kuwa watu waliyoathirika sio wagonjwa.

Huku hayo yakijiri maafisa katika mkoa wa Sindh -ambao ni moja ya maeneo yaliyo na viwango vya juu vya maambukizi ya HIV nchini Pakistan - wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha mlipuko huo.

Lakini hatua hiyo huenda isiwasaidie wale ambao wamepatika na virusi hivyo kwasababu itakuwa na athari kubwa kwa maisha yao.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii