Patrick Shanahan: Waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani asema taifa hilo limezuia vitisho vya Iran

Naibu waziri wa ulinzi nchini Marekani Patrick Shanahan alisema kuwa Marekani ilifanya busara sana

Kaimu waziri wa ulinzi nchini Marekani Patrick Shanahan alisema kuwa Marekani ilifanya busara sana

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Kaimu waziri wa ulinzi nchini Marekani Patrick Shanahan alisema kuwa Marekani ilifanya busara sana

Mashambulio yaliopangwa na Iran yamezuiwa na vitendo vya Marekani kulingana na naibu waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani Patrick Shanahan.

Marekani imeonya kuhusu tishio kutoka kwa Iran katika wiki za hivi karibuni na bwana Shanahan aliwaelezea wabunge katika mkutano wa faragha.

Hali ya wasiwasi imeongezeka huku Marekani ikipeleka vifaa vya kijeshi katika eneo la mashariki ya kati ili kukabiliana na vitisho hiyo visivyojulikana.

Siku ya Jumapili , rais Trump aliambia Twitter: Iwapo Iran inataka kupigana huo ndio utakuwa mwisho wake.

Amesisitiza sera mbaya dhidi ya Iran na tangu alipochukua mamlaka mwaka uliopita aliiondoa Marekani kutoka katika mkataba wa Kinyuklia na Iran pamoja na mataifa mengine matano yenye uwezo mkubwa duniani.

Mshauri wa maswala ya usalama nchini Marekani John Bolton amekuwa akipigania kubadilishwa kwa utawala wa Iran na amekuwa akitoa wito kwa Marekani kuilipua nchi hiyo.

Je Shanahan alisema nini?

Akizungumza na waandishi wa habari , alisema kuwa lengo la Marekani ni kuzuia badala ya vita.

Bwana Shanahan ambaye aliwahutubia wabunge akiwemo waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo alisema: Nadhani hatua zetu zilikuwa za busara na tumezuia mashambulio dhidi ya Marekani na hilo ndio muhimu.

''Naweza kusema kuwa tuko katika muda ambao vitisho viko juu na kazi yetu ni kuhakikisha kuwa hakuna uharibifu wowote utakaofanywa na Iran''.

Hakutoa maelezo yote kuhusu habari hizo muhimu zinazohusiana na swala hilo , lakini akaongezea: Natumai kwamba Iran inasikiliza.

Tupo katika eneo hili ili kuzungumzia mambo mengi, lakini sio kupigana na Iran.

Ripoti zinasema kuwa hotuba hiyo ilikumbwa na pingamizi mara nyengine na baada ya mkutano , baadhi ya wabunge wa chama cha Democrats waliwashutumu maafisa wa serikali kwa kubadilisha habari za kijasusi.

Kwa maoni yangu , hakukuwa na habari yoyote kwa nini tunapaswa kuanza mazungumzo ya kivita na Iran, alisema mbunge wa chama tawala Ruben Gallego.

Iran ilikubali kwamba kundi la JCPOA litapunguza mipango yake ya kinyuklia huku Iran nayo ikifaidika kwa kuondolewa vikwazo 2015 , na imeyataka mataifa ya magharibi kuheshimu mkataba huo licha ya Marekani kujiondoa.

Lakini shirika hilo la JCPOA linaonekana kuwa katika tishio.

Maafisa wa Iran walisema siku ya Jumatatu kwamba wameongeza kiwango cha uzalishaji wa madini ya Uranium -ijapokuwa ongezeko hilo ni la muda na ndani ya masharti ya makubaliano hayo.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Sanamu ya Sadam Hussein kufuatia kuondolewa kwa utawala wake

Je wasiwasi huo umesababishwa na nini?

Uhasama huo ulianza mapema mwezi huu , wakati Marekani iliondoa msamaha wake wa vikwazo kwa mataifa yanayonunua mafuta kutoka kwa Iran.

Uamuzi huo ulilenga kusitisha uuzaji wa mafuta wa Iran katika mataifa ya kigeni hatua ambayo ingelinyima taifa hilo chanzo cha mapato.

Bwana Trump aliirudishia vikwazo Iran baada ya kujiondoa katika mpango wa kinyuklia wa 2015 kati ya Iran na mataifa yenye uwezo mkubwa duniani ambao anataka ujadiliwe tena.

Siku chache baadaye, rais wa Iran Hassan Rouhani alisema kuwa taifa linasitisha vikwazo ilivyowekewa katika makubaliano hayo na kutishia kuongeza uzalishaji wa madini ya Uranium iwapo mataifa ya magharibi hayatachukua hatua za kulinda mafuta yake na sekta yake ya benki kutokana na athari za vikwazo vya Marekani kwa miezi miwili.

Baadaye ikulu ya Whitehouse ilitangaza kwamba Marekani ilikuwa inatuma meli ya kubeba ndege za kivita B-52 pamoja na kifaa cha kutungua makombora angani katika eneo la mashariki ya kati kutokana na vitisho vya Iran.

Je mataifa mengine yanasema nini?

"Ningeishauri Iran musidharau ari ya Marekani , alisema waziri wa maswala ya kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt.

''hawataki vita na Iran. lakini iwapo maslahi ya Marekani yatashambuliwa , watalipiza kisasi''.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Meli ya USS Abraham Lincoln imepelekwa mashariki ya kati

"Tunataka hali ya wasiwasi kupungua , kwasababu huu ni ulimwengu ambao mambo yanaweza kuchochewa kwa urahisi'' ,aliongez

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Saudia Adel al-Jubeir alisema kuwa Ufalme wa Saudia hautaki vita na utatumia kila njia kusitisha vita.

"lakini upande mwengine iwapo utataka vita , Ufalme huo utajibu na nguvu zake zote kujitetea na kulinda maslahi yake''.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Oman ambayo ilisimamia mazungumzo ya kisiri hapo zamani kati ya Marekani na Iran, alizuru Iran ili kujadiliana kuhusu maswala ya kieneo na waziri wa maswala ya kigeni nchini Iran Javad Zarif siku ya Jumatatu.ea.