Wanasayansi wagundua matumizi makubwa ya kemikali zinazoharibu 'paa la dunia' nchini China

home insulation Haki miliki ya picha Getty Images

Watafiti wanasema wamegundua vyanzo vikuu vya matumiazi ya 'kasi ya ajabu' ya kemikali sumu zinazoharibu tabaka ya ozoni.

Kemikali za CFC-11 zilikuwa maarufu kwa matumizi ya ujenzi kwa kuzipa joto nyumba hususani kwenye maeneo ya baridi lakini kukapitishwa makubaliano ya kusitisha matumizi hayo ifikapo mwaka 2010.

Hata hivyo, wanasayansi wamekuwa wakishuhudia kuzorota kwa kasi ya kusitisha ya kemikali hiyo katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Utafiti mpya wa kisayansi sasa unaonesha kuwa kuzorota huko kunatokana na matumizi mapya ya kemikali na gesi kwenye majimbo ya mashariki ya China.

CFC-11 ni moja ya kemikali za jamii ya chloroflurocarbon (CFC) ambazo hutumika kwa ajili ya kutengeza joto ama baridi tokea miaka ya 1930.

Hata hivyo iliwachukua wanansansi miaka mingi kugundua kuwa kemikali hizo ni hatari kwa anga la dunia na hutoboa tabaka la ozoni ambalo hulikinga dunia na mionzi mikali. Tabaka hilo hujulikana pia kama paa la dunia.

Tobo kubwa liligundulika kwenye tabaka hilo juu ya bara Antarctica katikati ya miaka ya 1980.

Jumuiya ya kimataifa ilikubaliana kuchukua hatua kwa kusaini Mkataba wa Montreal wa 1987 anbao ulipiga marufuku kwa kiasi kikubwa matumizi ya gesi hizo. Tafiti zinaonesha kuwa tobo la mhimili wa Aktiki litajiziba kufikia mwaka 1930 na lile la mhimili wa Antarctica kwenye mwaka 2060.

Mwaka 2018 timu ya watafiti ambayo inaangalia hali ya anga iligundua kuwa kasi ya uchafuzi imeshuka kwa 50% kuanzia 2012 .

Timu hiyo iligundua gesi hiyo ilikuwa ikitokea mashariki mwa Asia, na laini kama uzalishaji wake usingezuiwa kuna uwezekano mkubwa wa kuchelewesha kujitibu kwa tabaka la ozoni.

Utafiti wa kijasususi uliofanywa na Shirika la Uchubguzi wa Mazingira mwaka 2018 ulibainisha dhahiri kuwa China ndiyo ilikuwa ikitengeneza na kutumia gesi hizo. Uzalishaji huo pia unafanyika kienyeji na kinyume cha sheria.

Utafiti unabainisha kuwa, kwa ujumlaasilimia 40 mpaka 60 ya ongezeko la matumizi ya gesi hizo zinatokea mashariki mwa China.

Haki miliki ya picha Getty Images

Hesabu za kitafiti zinaonesha kuwa ongezeko la 110% uchafuzi wa anga katika maeneo hayo ya China baina ya mwaka 2014-2017 ikilinganishwa na mwaka 2008-2012.

Watafiti wakiongozwa na Dkt Matt Rigby, kutoka Chuo Kikuu cha Bristol, waliangalia kupitia mifumo ya kompyuta maeneo gani ya anga duniani yalikuwa yanatoa mionzi kwa wingi.

Kwa uchache gesi hizo pia zinaweza kuwa zinazalishwa katika maeneo ya India, Afrika ama Amerika ya kusini ambapo hakuna vituo vya uchunguzi.

Tani moja ya CFC-11 ni sawa na tani 5,000 za hewa chafu ya CO2. Hiyo inaonesha ni kwa kiasi gani kemikali na gesi hizo zilivyo na athari kubwa.

Serikali ya Uchina imesema inaendelea kuwachukulia hatua wazalishaji wa kemikali hizo ambao wamewaita ni wakora.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii