Tundu Lissu kurudi Tanzania Septemba ili kushiriki uchaguzi

Tundu lisu bamesema kuwa atawasili nchini Tanzania arehe saba mwezi wa tisa

Mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama cha Chadema na mnadhimu mkuu wa upinzani Tanzania Tundu Lissu ametangaza kwamba atarudi nchini humo tarehe saba mwezi wa tisa ikiwa ni miaka miwili tangu aliposhambuliwa.

Akizungumza kwa njia ya simu na kupitia runinga ya Chadema mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe katika makao makuu ya Chadema Lisu amesema kuwa atarudi nchini Tanzania siku hiyo ili kuadhimisha kushambuliwa kwake.

''Nitatua tarehe saba mwezi septemba 2019 kwenye ardhi ya tanzania kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nitakuwepo, alisema Tundu Lissu

Tangazo hilo liliwafurahisha sana wanachama wa chama hicho waliokuwa katika makao makuu ya chama hicho.

Mbowe amesema kuwa utaratibu wa mapokezi yake utapangwa na kutangazwa kitaifa.

Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma, katikati mwa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA kwa vyombo vya habari, tukio hilo lilitokea wakati mbunge huyo wa Singida Mashariki alipokuwa nyumbani kwake.

Tundu Lisu ni miongoni mwa wanasiasa wa upinzani nchini Tanzania ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Tanzania.

Ametangaza kwamba yuko tayari kuwania urais 2020 iwapo vyama vya upinzani vitamridhia kufanya hivyo.

Lisu adai shambulio lake lilikuwa la kisiasa

Toka wakati huo, Lissu na viongozi wengine wa upinzani wamekuwa wakilihusisha shambulio hilo na kazi yake ya siasa.

Wakati wa shambulio, Lissu hakuwa tu mnadhimu wa kambi rasmi bungeni Tanzania bali pia raisi wa chama cha wanasheria nchini humo.

Kwa kutumia kofia zake zote mbili, mwanasiasa huyo machachari alikuwa mwiba mkali wa ukusoaji wa serikali ya Magufuli.

Lissu alikuwa miongoni mwa wanansiasa wa upinzani waliopendelea kumuita Magufuli kuwa 'Dikteta Uchwara' ama kwa lugha ya kingereza'Petty Dictator'.

Baada ya shambulio hilo, alikimbizwa Nairobi kwa matibabu kisha Brussels Ubelgiji toka mwezi Januari mwaka 2018. Huko kote aliendelea kusisitiza kuwa serikali ya Magufuli ilikuwa na mkono kwenye shambulio dhidi yake.

Mada zinazohusiana