Maisha ya siri ya Mayaya wa Kiganda Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Kwanini wasichana wa Uganda wanavuka mpaka kutafuta kazi Kenya?

Nchini Uganda, wasichana wanaondoka nyumbani kujaribu kutafuta kazi za nyumbani katika mataifa jirani ikiwemo Kenya.

Lakini hatua hiyo ya kutafuta maisha huwafanya baadhi kuishia kunyanyaswa. Shirika la msaada nchini Kenya linatoa wito kuidhinishwa sheria za kuwalinda wafanyakazi wa nyumbani, au mayaya, kuhakikisha usalama wao.

Mwandishi wa BBC Nancy Kacungira katika BBC Africa Eye, amechunguza kwanini wasichana wanaoishi karibu na mpaka wa Kenya wanaondoka vijiini kutafuta kazi Kenya.