Utafiti: Aspirin inaweza kumpunguzia mtu hatari ya kupatwa na kiharusi au mshtuko wa moyo

Mwanamke akitumia dawa ya Aspirin Haki miliki ya picha Getty Images

Wagonjwa amabo wamewahi kupatwa na kiharusi kutokana na hali ya damu kuvuja kwenye ubongo wanaweza kukabiliana na hali hiyo kwa kutumia asprini.

Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni asprin inaweza kupunguza hatari ya mtu kupatwa na kiharusi au mshtuko wa moyo.

Madaktari wanasema dawa hiyo inafanya damu kuwa nyepesi hali ambayo imewafanya kuhofia kuitumia kama tiba kwa wagonjwa waliyo na matatizo ya kuvuja damu kwenye ubongo kwasababu huenda damu ikavuja zaidi.

Lakini utafiti huo uliyochapishwa katika jarida la matibabu la Lancet unasema kuwa dawa hiyo haiongezi hatari ya damu kuvuja kwenye ubongo.

Wataalamu hata hivyo wanasema "kuna haja" ya kubainisha hili kwa kufanya tafiti zaidi.

Wanapendekeza wagonjwa watumie asprin kulingana na ushauri wa daktari.

Manufaa ya Aspirin na madhara yake

Aspirin inajulika kwa ubora wake wa hali ya juu ya kutuliza maumivu na wakati mwingine hutumiwa kutuliza homa.

Lakini utumizi wa kila siku wadawa hiyo kiasi cha (75mg) unaweza kusaidia damu kuacha kushikana hali ambayo itamkinga mgonjwa kupatikana na mshtuko wa moyo ama kiharusi

Kiharusi mara nyingi husababishwa na tukio la damu kuganda kwenye mishipa mishipa au ubongo lakini zingine husababishwa kuvuja kwa damu kwenye ubongo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Vidonge vya Asprin

Kwasababu asprin husababisha damu kuwa nyepesi, wakati mwingine huenda ikamfanya mgonjwa kutokwa na damu nyingi kwa urahisi.

Asprin pia sio salama kwa kila mtu.

Inaweza pia kusababisha chakula kisisagike vizuri hali ambayo inaweza kumsbabishia mtu kupatwa na vidonda vya tumbo.

Usiwahi kumpatia mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 16 asprin bila ushauri wa daktari.

Inaweza kuwafanya watoto kupatikana na ugonjwa hatari unaojulikana kama Reye syndrome ambayo inaweza kuathiri (ini au ubongo).

Utafiti

Utafiti huo ambao ulihusisha wa 537 kutoka maeneo tofauti nchini Uingereza umebainisha kuwa watu waliyowahi kuwa na tatizo la kuvuja damu kwenye ubongo walipata nafuu baada ya kutumia dawa hii.

  • Nusu ya wagonjwa waliochaguliwa ili kuendelea na tiba hiyo walishauriwa kuachana nayo kwasababu walionesha dalili ya kukabiliwana hali ya hatari.
  • Katika kipindi cha miaka mitano utafiti huu watu 12 kati ya wale waliyoendelea kumeza tembe za dawa hiyo walipatatatizo la damu kuvuja kwenye ubongo huku watu 23 wakiepukana na tatizo hilo.
Haki miliki ya picha Getty Images

Matokeo ya utafiti huo yamewasilishwa katika kongamano la mwaka huu la Shirika la Ulaya la kukabiliana na maradhi ya kiharusi (ESOC 2019) mjini Milan.

Wataalamu wanasema nini?

Utafiti haujabainisha wazi ikiwa aspirin inaweza kumkinga mtu dhidi ya kiharusi siku za baadae lakini imehusishwa na kupunguza hatari ya kupa ugonjwa huo.

Pia haijapendekeza kuwa ni salama kumeza tembe za aspirin kila wakati.

Lakini amegusia kuwa baadhi ya wagonjwa walio na kiharusi kinachosabaabishwa na damu kuvuja kwenye ubongo- mhuenda wakanufaika na tiba ya kila siku kwa kutumia dawa hiyo.

Haijabainika wazi ikiwa utafiti huu utawasaidia wagonjwa wote.

Mtafiti mkuu, Prof Rutsam Salman, kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh, alisema: "Kwa sasa watu hawajui kitu sahihi cha kufanya.

"Madaktari wanahofia kuwapatia aspirin ana dawa zozote zinazokaribiana na aspirin-watu waliyo na aina hii ya kiharusi.

"Muongozo wa tiba wa Uingereza na Ulaya haujatoa mapendekezo yoyote kwasababu haujapata ushahidi wa kutosha.

"Nadhani sasa tumethibitisha usalama wa dawa hii kutokana na matokeo haya.

"Bila shaka ni salama kupeana aspirin ."

Haki miliki ya picha Getty Images

Prof Salman amependekeza utafiti zaidi ufanywe ili kupata hakikisho kamili kwamba aspirin huenda ikapunguza hatari ya damu kuvuja ndani ya ubongo au kuganda.

Prof Metin Avkiran, kutoka waakfu wa British Heart Foundation, ambao umefadhili utafiti huu, amesema: "Karibu thuluthi moja ya watu waliyo ma matatizo ya damu kuvuja kwenye ubongo au kiharusi kilichosababishwa na hali hiyo wanatumia dawa kama vile kupunguza hatari ya kupatwa na mshtuko wa moyo.

"Sasa tumepata mwelekeo imara wa kuendeleza mbele tiba hii ambayo ina uwezo wa kuokoa maisha ya watu wengi."

Mtu yeyote aliye na hofu ya kubadilisha utaratibu wa matibabu anashauriwa kufuata maelezo ya dakitari.

Kujiepusha na Kiharusi

Unaweza kujikinga na hatari ya kupata kiharusi kwa:

  • Kuzingatia lishe bora
  • Kufanya mazoezi ya mara kwa mara
  • Kujiepusha na uvutaji sigara
  • Unywaji pombe wa kupindukia

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii