Botswana imeondoa marufuku ya uwindaji tembo

Elephant at the Okavango Delta Haki miliki ya picha Getty Images

Botswana imeondoa marufuku ya uwindaji tembo kutokana na ongezeko la mzozo kati ya binadamu na wanyama ambao wanaharibu mashamba yao.

Wakosoaji wa marufuku hiyo iliyowekwa mwaka 2014, wanasema udhibiti huo ulikuwa unawaathiri wakulima wadogo na watu waliyokua wakinufaika na uwindaji wa mnyama huyo.

Hatua hiyo huenda ikakosolewa vikali na wanaharakati wa uhifadhi wa wanyama ambao wanaamini imetokana na sababu za kisiasa.

Kuna hofu uamuzi huo utaathiri sifa ya nchi hiyo kimataifahaliaambayo pia huenda ikaathiri mapato yanayotokana na utaliiambao ni chanzo kikubwa cha mapato ya kifeni kwa taifa hilo baada ya uchimbaji madini ya Almasi.

Serikali imesema nini?

Mwezi Juni mwaka jana Rais Mokgweetsi Masisi alibuni kamati ya kuchunguza umpya marufuku hiyo ambayo iliwekwa na mtangulizi Ian Khama mwaka 2014.

"Visa vya tembo kuwashambulia watu vinazidi kuongezeaka hali ambayo inatia hofu," ilisema taarifa ya Wizara ya Mazingira, Mali asili, Uhifadhi na Utalii.

Haki miliki ya picha Getty Images

Wizara hiyo iliongeza kuwa itahakikisha uwindaji wa tembo unafanywa kwa ''utaratibu'' maalum.

Wataalamu wa uhifadhi wanasema mbuga za wanyama zinakabiliwa na changamoto za kiekolojia kwasababu wanyama wamekua wengi kupita kiasi katika hifadhi zao, maji yamekua haba na malisho au chakula chao pia kimepungua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Utafiti unaonesha kuwa tembo wanasafiri mbali na umbali wa safari zao umeendelea kuongezeka.

Haki miliki ya picha Inpho
Image caption Botswana inajivunia kuwa na thuluthi tatu ya tembo barani Afrika

Tembo wanaweza kusababisha uharibifu mkubwa wanapovamia mashamba na wakati mwingine wanaweza kuua watu wakijaribu kuwafukuza.

Idadi kubwa ya tembo nchini Botswana wanapatikana katika maeneo ya mpaka wa Namibia, Zambia na Zimbabwe.

Wanaharakati wa kimataifa wa uhifadhi wamekuwa wakishinikiza marufuku ya uwindaji tembo kama njia ya kukabiliana na uwindaji haramu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii