Arthur: Runinga ya Marekani yakataa kuonyesha katuni ya ndoa ya jinsia moja Alabama

Picha ya kipindi cha watoto kwa jina Arthur Haki miliki ya picha WGBH & PBS KIDS
Image caption Wengi walikipongeza kipindi hicho kwa kuonyesha ndoa ya jinsia moja katika runinga ya watoto

Runinga moja ya Umma katika jimbo la Alabama nchini Marekani imekataa kupeperusha hewani kipindi cha ndoa ya wanasesere wapenzi wa jinsia moja.

Sehemu ya kwanza ya kipindi hicho chenye msururu wa sehemu 22 ya kipindi cha watoto cha Authur kinashirikisha muigizaji bwana Ratburn akimuoa mpenzi wake Patrick.

Hatahivyo runinga hyo ilipeperusha hewani sehemu ya zamani ya kipindi hicho na kutangaza kwamba haina mpango wa kupeperusha hewani sehemu hiyo.

Mkurugenzi wa vipindi Mike McKenzie alisema kuwa kukipeperusha kipindi hicho kungevunja imani ya wazazi katika runinga hiyo.

Katika taarifa, bwana McKenzie alisema kuwa wazazi wana imani kwamba watoto wao wanaweza kutazama runinga hiyo bila ya usimamizi na kwamba watoto wadogo zaidi wanaweza kutazama bila ya wazazi wao kujua.

Watengenezaji wa kipindi hicho WGBH na watangazaji PBS walizielezea steshini katika jimbo hilo mnamo mwezi Aprili kuhusu sehemu hiyo ya kipindi na bwana McKenzie alisema hivyo ndivyo walivyoamua kutopeperusha kipindi hicho.

Kipindi cha Arthur ni msururu wa vipindi kwa ushirikiano wa Canadian/Marekani ambacho kilianzishwa 1996 kuhusu katuni mwenye umri wa miaka minane anthropomorphic aardvark kwa jina Arthur Read na marafiki zake ambao wanaishi katika mji usiokuwepo wa Elwood.

Runinga hiyo awali ilikataa kupeperusha sehemu ya 2005 ya kipindi hicho ambayo ilimuonyesha Buster , Sungura ambaye alikuwa akimtembelea msichana mwenye mama wawili.

Mwalimu kwa jina Misty Souder aliambia tovuti ya habari ya AL.com kwamba yeye na mwanawe walisikitishwa kwamba kipindi hicho hakikupeperushwa hewani na kwamba alikuwa amewasiliana na runinga hiyo kukihusu.

''Sikudhania kwamba nitapigania kuhusu kuonyeshwa kwa ndoa ya wapenzi wa jinsia moja , lakini hapa ndipo tulipofikia'', alisema.

Kura ya maoni ya 2018 iliofanywa na Gallup ilionyesha kuwa asilimia 46 ya watu mjini Alabama walijitambulisha kuwa wahafidhina, ikiwa ni wapili kwa wingi baada ya jimbo la Mississipi katika majimbo yote 50.

Mapema mwezi Mei, Alabama ilipitisha sheria iliopiga marufuku uavyaji mimba katika maswala ya ubakaji na kujamiana na ndugu wa karibu, ikiwa hatua ya hivi karibu ya Jimbo la Marekani kuzuia uavyaji mimba.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii