Uchaguzi Malawi: Kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera achukua uongozi wa mapema

Rais Peter Mutharika (kulia) inakabiliwa na upinzani kutoka kwa Lazarus Chakwera (kushoto) na Saulos Chilima (kati) Haki miliki ya picha AFP

Kiongozi wa upinzani nchini Malawi amechukua uongozi wa mapema katika uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo mwezi Mei 21, kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.

Lazarus Chakwera , kiongozi wa chama cha upinzani cha Malawi Congress Party MCP amejipatia kura 533,217 ambayo ni sawa na asilimia 37.65.

Anafuatiwa kwa karibu na rais wa sasa Peter Mutharika ambaye ana kura 524,247 ikiwa ni asilimia 37.1 huku makamu wa rais Saulos Chilima wa United Transformation Movement akiwa wa tatu na kura 293,978 ambayo ni asilimia 20.76.

Kiongozi wa chama cha zamani zaidi nchini Malawi Lazarus Chakwera amesema kuwa matokeo hayo ya mapema yanampatia uongozi katika uchaguzi huo.

Amesema kwamba kuna jaribio la baadhi ya watu wasiojulikana kuingilia matokeo ya uchaguzi huo yanayopeperushwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha uchaguzi mjini Blantyre akiapa kwamba hatokubali uchakachuaji wwote.

Lakini tume ya uchaguzi nchini humo imetoa wito wa kuwepo kwa utulivu ikisisitiza kuwa ndio yenye uwezo wa kutangaza matokeo hayo.

Uchaguzi huo umekumbwa na ushindani wa karibu kati ya rais Peter Mutharika , makamu wake Saulos Chilima na Chakwera ambaye anakiongoza chama cha Malawi Congress party.

Katika uchaguzi wa 2014 , Chakwera alipoteza kwa karibu dhidi ya rais Mutharika na akashindwa kupinga uchaguzi huo mahakamani.

Tume ya uchaguzi ina hadi siku nane kutangaza matokeo hayo .

Hatahivyo imekiri kwamba inakabiliwa na changamoto za kiufundi katika utangazji wa matokeo hayo.

Hatahivyo inasema kuwa ina imani kwamba itatoa matokeo yalio huru na haki.

Takriban raia milioni 6.8 wa Malawi walisajiliwa kushiriki katika uchaguzi huo kumchagua rais mpya , mbunge mpya na madiwani.

Haki miliki ya picha AFP

Hii ni mara ya kwanza kura kujumlishwa na kutumwa kwa njia ya kiilektronic.

Zaidi ya wapiga kura milioni saba walipiga kura kumchaguza rais na wabunge na madiwani Jumanne Mei 21 katika uchaguzi ambao hauwezi kutabirika katika historia ya nchi hiyo.

1. Makamu wa rais asimama dhidi ya Rais

Maswali mengi kuhusu iwapo afya ya rais Peter Mutharika inamruhusu kugombea muhula mwingine yamezusha mgawanyiko na makamu wake wa rais, Saulos Chilima.

Chilima aliteuliwa na rais Mutharika kama mgombea mwenza wake katika uchaguzi uliopita mnamo 2014. Lakini mwaka uliopita shemegi yake rais, Callista Mutharika, alipendekeza kwamba umri wa kiongozi huyo , miaka 78, ni mkubwa kwa yeye kuchagulia tena na kwamba sasa atoe fursa kwa makamu wake aliye na umri wa miaka 46.

Pendekezo hilo lilipingwa na wafuasi wenye ushawishi katika chama tawala cha Democratic Progressive Party (DPP).

Kulizuka mgawanyiko wa chama hicho pande mbili, na hatimaye Chilima aliishia kuanzisha chama cha UTM, huku akisalia kuwa makamu wa rais nchini.

Haki miliki ya picha AFP

Haijulikani wazi iwapo Bi Mutharika wana sikizana na shemegi yake - hivi karibuni hakuhudhuria uzinduzi wa sanamu la marehemu mumewe Bingu wa Mutharika. Anagombea ubunge kupitia chama hicho cha makamu wa rais UTM.

Chilima anaonekana kama ishara ya mabadiliko kwa raia nchini Malawi wanaotamani mageuzi.

Umri mdogo wa Chilima huenda ukawa na manufaa kwake, wakati raia walio na umri wa katiya miaka 18 na 34 wakiwa wanajumlisha 54% ya wapiga kura nchini.

2. Mke wa makamu wa rais 'afoka' kumtafutia mumewe kura

Mkewe Chilima, Mary, ameingia uwanjani akitafuta ushindi wa vijana kwa kuanza kuimba nyimbo za kufoka foka au rap.

Katika kanda ya video, kando na kufoka, anadensi na kutumia mistari inayofahamika kwa vijana huku akionekana kuvaa nguo kama wao.

Amewasilisha pia matangazo ya biashara yanayowalenga wapiga kura wanawake.

Wagombea ni kina nani?

Wagombea saba wapo kwenye debe katika uchaguzi wa urais Malawi, lakini watatu ndio wanaopigiwa upatu kuwa na nafasi ya kushinda:

Peter Mutharika - Democratic Progressive Party - rais wa sasa anayegombea muhula wa pili

Lazarus Chakwera - Malawi Congress Party - Anatumai kufufua utajiri wa chama tawala cha zamani

Saulos Chilima - UTM Party - makamu wa rais hivi sasa anayewania kiti dhidi ya mku wake

3. Hakuna wagombea wanawake wa urais

Haki miliki ya picha AFP

Licha ya kwamba wanawake ni 56% ya wapiga kura nchini, hakuna mwanamke anayegombea urais nchini.

Rais wa zamani Joyce Banda, aliyeshndwa na Mutharika mnamo 2014, alijitoa katika kinyang'anyiro hicho kumuunga mkono Lazarus Chakwera wa chama cha Malawi Congress Party (MCP).

Uchaguzi wa ubunge na udiwani pia unafanyika kwa pamoja katika uchaguzi huuu. zaidi ya wanawake 300 wanagombea viti katika bunge la uwakilishi wa viti 153. Huku mamia wengine wakigombea katika viti vya serikali za mitaa.

Takriban wiki moja ikiwa imesalia kwa uchaguzi mkuu kufanyika, kumekuwa na uvumi uliosambaa kwamba rais Mutharika huenda ni mgonjwa mahututi au amefariki. Hili lilifuatwa kwa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ofisini mwake iliosema kwamba anakatiza mikutano mingine ya kampeni ili "kushughulikia mambo mengine muhimu zaidi".

Picha ya ndege ya ambulensi ya Afrika kusini, iliyokuwa katika uwanja mkuu wandege wa nchi hiyo, ilianza kusamba aktika mitandao ya kijamii iliyoongeza chumvi uvumi huo.

Mutharika alizuka upya katika kampeni siku mbili baadaye na kuwakejeli upinzani.

Alisema kwamba badala ya yeye kufa, ni wapinzani ake watakaoteseka kwa kifo cha kisiasa uchaguzi utakapofika.

"Je nimekaa kama maiti kwenu?" aliwauliza wafuasi wake.

Kumeshuhudiwa ghasia kwa kiasi fulani lakini kwa ukubwa kampeni zimekuwa za amani.

Hakuna duru ya pili ya uchaguzi katika uchaguzi huo wa rais Malawi - mgombea atakayejinyakulia kura nyingi ndiye mshindi.

5. Mauaji ya walemavu wa ngozi - Albino

Suala jingine lililogubika kampeni nchin ini mfululizo wa mauajai ya watu wenye ulemavu wa ngozi - Albino- kufuatia kuwadia kwa uchaguzi mkuu.

Kuna wasiwasi kwamba huenda suala hilo likaharabu nafasi ya makamu wa rais.

Ripoti ya Umoja wa matiafa imeashiria kwamba mashambulio na mauaji ya walemavu wa ngozi huongezeka wakati wa uchaguzi "kutokanana imani potofu kwamba viungo vya walemavu vinaweza kuleta bahati nzuri na nguvu za kisiasa na hutumika katika visa vya uchawi".

Vyama vya upinzan vinautuhumu utawala wa Mutharika kwa kutowajibika ipasavyo kusitisha mashambulio hayo.

Rais analikana hilo na ameunda tume ya uchunguzi, kuchunguza mauaji hayo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii