Eric Omondi athibitisha kutengana na mpenzi wake Chantal Grazioli

Mckekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya Eric Omondi

Mchekeshaji maarufu Afrika mashariki Eric Omondi amewachana na mpenzi wake wa siku nyingi Chantal Grazioli.

Uvumi wa kuvunjika kwa penzi lao la miaka minne ulisambaa katika mitandao ya kijamii kabla ya Omondi mwenyewe kuthibitisha rasmi katika mtandao wake wa Instagram.

Tukio hilo linajiri wakati ambapo mchekeshaji huyo anazidi kuvutia mashabiki wengi katika sekta hiyo ya uchekeshaji huku wengi wakihoji ni nini haswa kilichosababisha kuvunjika kwa mahaba yao.

Katika chapisho lake refu katika mtandao huo wa Instagram, Omondi ameandika kwamba anamtakia heri Grazioli huku akiendelea na awamu yake mpya ya maisha bila yeye huku akisisitiza kuwa mwanadada huyo alibadilisha maisha yake.

''Nilikutana nawe ukiwa na umri wa miaka 19.... Nimekuwa kwa miaka minne na nusu....tuliishi na kuwa na wakati mzuri zaidi katika maisha naye. Ulibadilisha maisha yangu kabisa....wakati unapoanza maisha yako mapya na mimi au bila mimi nakutakia heri mpenzi wangu. Njia iliotuleta pamoja sasa inatupeleka maeneo tofauti na unapoenda njia tofaut nakutakia heri katika maisha'', aliandika.

Na kutokana na visa vingi vya uhalifu wa kimapenzi...Eric Omondi alitoa ushauri wa bure kwa wanaume kuhusu jinsi wanavyotakiwa kufanya kufuatia kuvunjika kwa mahusiano yao na wapenzi wao.

''Kwa wale vijana wanafikiria kuuana baada ya mapenzi kuisha , nataka hili liwe funzo kweny nyote. Hauwezi kum'miliki mpenzi wako na mara nyingine mambo huenda visivyo.

Alielezea kwamba wote wako salama, baada ya kuwa marifiki mwanzoni.

''Nakuombea mungu kwamba atakulinda. Namuomba akuongoze.... nataka kukwambia kwamba...nitakuwepo kila utakaponihitaji wakati wowote na muda wowote. Unapoelekea mpenzi wangu nakuombea ung'are kama kama malaika ulivyo. Ntakuenzi kila mara...kila wakati. Wewe ni kitu bora zaidi katika maisha yangu!! Na kwa wale wadau wadaku, Mimi na Chantal hatuna tatizo . Sisi tulikuwa marafiki kabla ya kuwa wapenzi na urafiki wetu utasalia kwa maisha.."

Haki miliki ya picha Eric Omondi/Instagram

Na baada ya ujumbe huo mmoja wa mashabiki wake katika mtandao wa instagram walianza kutoa mawazo yao kufuatia hatua hiyo ya Eric Omondi

Shabiki wake kwa jina Akotheekenya: Nakupenda kwa kweli , ndugu yangu , wapenzi wengi wanafaa kujua kwamba penzi haliishi na iwapo unampenda mwanchilie.... nalia machozi ya hisia tofauti.

Mwengine kwa jina kansiime alisema: unafanya mapenzi kuwa mazuri zaidi

Wengine walimwamba kwamba amekuwa akimpenda mwanadada huyo zaidi ya anavyompenda.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii