Ethiopia yaomba radhi kwa kutoa ramani iliyojumuisha Somalia katika mipaka yake

Wizara ya Mambo ya nje ya Ethiopia imesema haielewi jinsi ramani hiyo "ilivyoingia katika tuvuti yake" Haki miliki ya picha Ministry of Foreign Affairs of Ethiopia
Image caption Wizara ya Mambo ya nje ya Ethiopia imesema haielewi jinsi ramani hiyo "ilivyoingia katika tuvuti yake"

Wizara ya mambo yan je ya Ethiopia imeomba radhi baada ya ramani ya Afrika iliyochapishwa katika tuvuti yake kuonesha taifa jirani la Somalia limejumuishwa kwatika mipaka yake.

"Tunaomba radhi kwa mkanganyiko huo na usumbufu ambao huenda umesababishwa na tukio hilo," ilisema taarifa ya wizara hiyo.

Somalia ilikuwa imeondolewa kabisa katika ramani hiyo lakini eneo la Somaliland lililojitangazia uhuru wake na ambalo halitambuliwa Kimataifa- lilioneshwa.

Majirani hao walikuwa mahasimu wa jadi ambao walizozania mipaka.

Lakini uhusiano kati ya mataifa hayo mawili umeimarika tangu Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuingia madarakani mwaka jana na kutuliza taharuki iliyokua ikiendelea katika eneo hilo.

Matukio: Ethiopia na Somalia

  • 1964 na 1977: Mapigano yalizuka mara mbili kati ya mataifa hayo baada ya Ethiopia kuvamia eneo la Ogaden linalokaliwa na Wasomali
  • 1988: Mkataba wa amani ulitiwa saini , mika mitatu baadae Somalia ikatumbukia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
  • 1996: Vikosi vya Ethiopia viliingia Somalia kukabiliana na wapiganaji wa kiislam katika mji wa Luuq
  • 2006: Wanajeshi wa Ethiopia waliingilia kati mapambano ya kung'o utawala wa wanamgambo wa Kiislam nchini Somalia
  • 2009: Wanajeshi wa Ethiopia waliondoka rasmi nchini Somalia, lakini walisalia nchini humo hadi wa leo kama sehemu ya kikosi cha kulinda usalama cha Umoja wa Afrika kilichopelekwa kupambana na wanamgambo wa kundi la al-Shabab.
  • June 2018: Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alizuru Somalia kuimarisha uhusano kati ya mataifa hayo mawili.
  • Oct 2018: Serikali ya Bw. Abiy ilitia saini mkataba wa kufikia amani na wanamgambo wanaopigania eneo laOgaden.

Ramani hiyo ilizua gumzo kali katika mitando ya kijamii, huku Wasomali wakisema kuwa hatua hiyo imeweka bayana mpango wa Ethiopia kutaka kunyakua taifa lao.

Wengine walilipiza kisasi kwa kushapisha mtandaoni ramani yao inayojumuisha Ethiopia ndani ya Somalia.

Wengine waligundua makosa mengine katika ramani hiyo iliyochapishwa katika wavuti wa Wizara ya Mambo ya nje ya Ethiopia, kwa mfano, ilionesha taifa la Congo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kama taifa moja na haikuonesha Sudan Kusini, ambaye ilitenganishwa na Sudan mwaka 2011.

Serikali ya Somalia haikujatoa tamko lolote rasmi kuhusiana na tukio hilo.

Waziri wa zamani wa Mambo ya nje Yusuf Garaad amepokea hatua ya kuondoa ramani hiyo, lakini akahoji kwanini ilichorwa.

Katika taarifa yake Wizara ya Mambo ya nje ya Ethiopia ilisema kuwa haina uhakika jinsi ramani hiyo ilivyochapishwa katika tuvuti yake, ambayo haitumiki kwa sasa, lakini ikaongeza maafisa wake wa kiufundi wanafanya kila juhudi kuhakikisha usalama wake.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii