China: Apigwa faini kwa kujikuna huku anaendesha gari

Mr Liu scratching his face Haki miliki ya picha Sina Weibo

Mwanaume mmoja kutoka mashariki mwa China amepigwa faini mara baada ya kamera ya trafiki kumpiga picha akiwa anajikuna usoni.

Kwa mujibu wa chapisho la Jilu Evening, limeandika kuwa Liu alikuwa anaendesha gari siku ya jumatatu katika jimbo la Shandong na huku akiwa anajikuna wakati anapita katika kamera ya trafiki.

Ghafla alipokea ujumbe unaomwambia kuwa amevunja sheria barabarani kwa kuendesha gari huku anaongea na simu.

Picha ya kosa ambalo alikuwa amelifanya liliambatanishwa katika ujumbe huo wa kuvunja sheria.

Aliambiwa kuwa ataondolewa pointi mbili katika leseni yake na vilevile alitakiwa kulipa dola saba kama faini.

"Huwa nawaona watu mitandaoni wakiwa wamekatwa kwa kosa la kuendesha huku wamewashika watu wengine labda miguu lakini mimi nimekamatwa kwa kujishika mwenyewe ndio nimeonekana kuwa nimevunja sheria, inashangaza'!"

Mshitakiwa huyo amesema kuwa anajaribu kuongea na mamlaka ili kupata suluhisho ya tatizo lake .

Haki miliki ya picha Sina Weibo
Image caption Liu aliweka picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii

Gazeti la Global Times limesema kuwa trafiki polisi wamefuta risiti ya makosa waliomwandikia na kumwambia kuwa kamera yao huwa inarekodi mwendo wa dereva moja kwa moja, ndio maana kunikuna kwake uso kulimweka matatani na kuonekana kama anaongea na simu.

Picha yake imezua gumzo mtandaoni huku wengine wakiwa wakiwa wanaweka kejeli ya kesi yake na wengine kutoa maoni juu ya namna faini zinavyotolewa .

"Mfumo huo unahaibisha sana, watu wanakuwa hawana faragha."

"Je, hakuna umuhimu kwa wachina kuwa na faragha?" mtu mwingine aliuliza.

Kamera zaidi ya milioni 170 zipo nchini China na nyingine milioni 400 zinatarajiwa kuwekwa mwakani.

Kamera hizo zimewekwa huku zikiwa na teknolojia inayoweza kutambua muonekano wa watu na kujua umri , jinsia na eneo walilotoka.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii