'Maziwa ya ng'ombe yanaweza kumuua mwanangu'

Evie
Image caption Evie Kinsella ana mzio(allergy) wa maziwa ya ng'ombe

Ni kawaida kwa watoto wengi wenye umri wa miaka mitano kupenda kucheza muziki kama ilivyo kwa Evie Kinsella .

Evie ni mtoto ambaye anapenda kucheza na kuchezea karibu kila kitu, kupanda kwenye miti na kuokota majani.

Lakini yeye kwenda kwenye duka la kahawa kunaweza kumsababishia madhara makubwa.

Mtoto huyu ana mzio wa maziwa ya ng'ombe na hali yake hubadilika hata akisikia harufu tu .

"Inanisikitisha kwa sababu siwezi kufanya kila kitu, kama vile kula meza moja pamoja na wenzangu shuleni au kwenda kwenye sherehe na kula chakula kama wenzangu wanavyofanya," Evie alisema

"Ninakuwa na wasiwasi watu wanaponisogelea karibu wale ambao wametoka kunywa maziwa.

Wanaweza kunifanya niteseka sana.

Madhara ambayo ninapata huwa yananifanya nitishe na kujisikia vibaya sana."

Evie alikuwa akiugua mara kwa mara wakati alipokuwa mtoto lakini ni baada ya kunywa maziwa ya mtindi, akiwa na miezi sita alilazwa kwa sababu ya mzio.

"Alikuwa akipiga kelele sana, sura yake yote inabadilika kwa kuvimba , muonekano wake ulikuwa sawa kama wa muigizaji filamu za kutisha," Mama yake Katie alisimulia.

Image caption Mtoto huyu amelazwa mara kadhaa kutokana na mzio

Mwezi mmoja baadae, Katie alienda kwenye duka la kahawa pamoja na rafiki zake, na akiwa Evie, na kwa sabubu kulikuwa kunasikika harufu ya maziwa matatizo yakaanza tena. Mwisho wa siku alilazwa kwa sababu alishindwa kupumua.

Hali hiyo imemtokea mara nyingi na hata imebadilisha maisha yetu.

Mara nyingi tunaacha kufanya vitu fulani ili kuepusha mtoto wetu asidhulike.

Kwa mujibu wa tafiti asilimia 7.5 ya watoto wana mzio wa maziwa ya ng'ombe , kitu ambacho kinawafanya washindwe kula vyakula vingi.

Evie hupata mzio akila vyakula vingine pia kama karanga ila maziwa peke yake ndio huwa yanamtesa zaidi.

Image caption Evie huwa hali mayai na karanga

Kuna watoto ambao wanakufa kutokana na mzio wa maziwa ya ng'ombe ingawa hakuna ambaye anajali , Katie alisema

Madhara anayopata huwa yananisononesha sana, huwa tunalia mara kwa mara ingawa kila mtu huwa anasema ni kitu cha kawaida. Wakati mimi huwa ninajihisi kuchanganyikiwa mtoto akianza kuumwa."

Haki miliki ya picha Adam Robertson
Image caption Lauren Gordon akiwa na mwanae

Mtaalamu wa afya amemuhamasisha Lauren kumpa mwanae maziwa ya fomula lakini mtoto anakataa kuyanywa kwa sababu hajapenda ladha yake.

Mtoto wake Dilan alikuwa anapata madhara baada ya kunyonya alikuwa anaanza kupiga chafya.

Lauren aliweka orodha ya vyakula ambavyo ni salama ambavyo haviwezi kumdhuru mtoto wake na kushangazwa kuwa karibu kila chakula kilikuwa na mchanganyiko wa maziwa.

Nilianza kuwa mtaalamu wa kusoma vitabu , mpaka nikaanza kuwatumia taarifa wazazi wengine ambao wanahangaika na tatizo kama langu kupitia mitandao ya jamii."Lauren alifungua blogu na kurasa za Facebok na Instagram na maelfu ya wazazi wanamfuatilia na kusimulia visa vyao kila mmoja.

Haki miliki ya picha Adam Robertson
Image caption Lauren anatamani kuwa mzio wa maziwa ya ng'ombe utakuja kueleweka siku zijazo

"Baadhi yao ni kama wamechanganyikiwa na wapo katika kiza. Huwa hawapati ushauri mzuri.

wengine huwa wanataka kuwa watoto wenye afya nzuri na furaha lakini hawataki kujua nini cha kufanya."

Anatamani kuwa mzio unaweza kuja kueleweka katika siku zijazo kwa wazazi wengine.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii