Ni kwanini Wayahudi wamekatazwa kuvaa kofia zao Ujerumani?

Kofia zinazovaliwa utosini - au kippa - huvaliwa na wanaume wa Kiyahudi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kofia zinazovaliwa utosini - au kippa - huvaliwa na wanaume wa Kiyahudi

Kamishna wa kupambana na ubaguzi wa chuki za kijamii nchini Ujerumani amewataka Wayahudi kuepuka kuvaa kofia za kiyahudi katika maeneo ya umma .

Felix Klein amewaonya Wayahudi waache kuvaa kofia zao zinazofahamika kama kippa katika baadhi ya maeneo ya nchi kufuatia kuongezeka kwa chuki dhidi ya wayahudi nchini Ujerumani.

Amesema maoni yake juu ya suala la chuki kwa Wayahudi "yamebadilika ikilinganishwa na yalivyokuwa awali ".

Rais wa Israeli Reuven Rivlin amesema wito huo unamaanisha "kukiri kwamba, kwa mara nyingine tena, Wayahudi hawako salama katika ardhi ya Ujerumani".

Ongezeko kubwa la idadi ya makosa ya chuki dhidi ya Wayahudi liliripotiwa mwaka jana.

Huku takwimu rasmi zikionyesha matukio ya uhalifu wa chuki dhidi ya Wayahudi yakifikia hadi 1,646 katika mwaka 2018 - idadi hiyo ilkiwa ni sawa na ongezeko la 10% ikilinganishwa na mwaka jana.

Mashambulio ya moja kwa moja dhidi ya Qayahudi nchini Ujerumani pia yaliongezeka katika kipindi hicho, huku matukio ya kuwapiga Wayahudi 62 yakirekodiwa, ikilinganishwa na mwaka jana ambapo watu 37 ndio waliopigwa mwaka 2017.

Akizungumza na gazeti la Handelsblatt, Waziri wa sheria wa Ujerumani Katarina Barley alisema kuwa kuongezeka kwa uhalifu wa chuki dhidi ya Wayahudi ni "aibu kwa nchi".

Bwana Klein alisema nini?

"Siwezi kuwashauri Wayahudi kwamba wavae kofia zao zinazofunika utosini kwa wakati wowote na kila mahali nchini Ujerumani," aliliambia gazeti la Funke.

Bwana Klein alisema kuwa "kuondolewa agizo linalowataka wayahudi wawe makini pamoja na kuacha kuwa na ukiukaji wa maadili" ya jamii linaweze kuwa kwa sasa si muhimu kutokana na ongezeko kubwa la uhalifu wa ubaguzi dhidi ya Wayahudi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Utafiti umeonyesha kuwa Wayahudi wanaoishi katika nchi mbali mbali barani Ulaya wamekuwa na hofu kubwa hivi karibuni kutokana na chuki inaypoendelea kuongezeka dhidi yao

Intaneti, mitandao ya kijamii na "upinzani usiosita dhidi ya utamaduni wa kumbukumbu ya mauaji ya wayahudi " huenda vimechangia ongezeko la visa hivyo, alisema.

Aidha aliwatolea wito maafisa wa polisi, waalimu na mawakili kupata mafunzo ya kuweka bayana "kile kinachokubalika na ambacho hakikubaliki " wakati "wanapokabiliana na uhalifu dhidi ya Wayahudi".

Kauli zake zimekuja wiki kadhaa baada ya mmoja wa wataalamu wa ngazi ya juu wa masual ya sheria za ubaguzi dhid ya Wayahudi kusema kuwa ubaguzi bado upo sana'' mio0ngoni mwa jamii za Ujerumani.

"Ubaguzi dhidi ya Wayahudi umekuwepo. Lakini ninadhani hivi karibuni, umetajwa sana , kuongezeka na wa kiwango kibaya zaidi" Claudia Vanoni aliliambia shirika la habari la AFP.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Israeli Reuven Rivlin amesema kwa Wayahudi hawatalipiza kisasi kutokana na mashambulio ya chuki dhidi ya Wayahudi nchini Ujerumani

Rais wa Israel amejibu vipi?

Bwana Rivlin alisema kuwa "ameshitushwa " na onyo la Bwana Klein na analichukulia kama " kuukubali ubaguzi dhidi ya Wayahudi".

"Hatutasalimu amri ,hatutayumbishwa na hatutajibu ubaguzi dhidi ya Wayahudi kwa kushindwa, na kutarajia kuwataka washirika wetu wachukuehatua kwa njia sawa na iliyotumiwa ,"amesema rais wa Israeli.

Alitambua " Msimamo wa maadili wa serikali ya Ujerumani na kujitolea kwake kuilinda jamii ya Wayahudi".

Ni kwanini Chuki dhidi ya Wayahudi imeongezeka?

Makundi ya Wayahudi yameonya kuwa kuongezeka kwa umaarufu wa makundi yenye itikadi za mrengo wa kulia kunachochea chuki dhidi ya Wayahudi pamoja na jamii nyingine za walio wachache kote barani Ulaya.

Tangu mwaka 2017, chama cha mrengo wa kulia nchini Ujerumani (AfD) kimekuwa ndio chama kikuu cha upinzani. AfD kiko wazi kwamba kinapinga uhamiaji lakini chama hicho kinakana kuwa kinaendelesha kampeni ya kusambaza maoni ya chuki.

Hata hivyo, kauli kadhaa zinazotolewa na wanasiasa wa chama hicho, ikiwemo iliyotolewa kwa ajili ya kumbukumbu ya mauaji ya Holocaust, zimeibua ukosoaji mkubwa kutoka kwa makundi ya Wayahudi pamoja na wanasiasa wengine

Mwaka jana, utafiti wa maelfu ya Wayahudi wa Ulaya ulifichua kwamba wengi wamekuwa wakiendelea kuwa na hofu kubwa juu ya chuki dhidi ya yao.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii