Hedhi kwa wasichana hawa ni karaha
Huwezi kusikiliza tena

Wasichana wa Turkana hukosa masomo wakati wa hedhi

Wakati dunia inapoadhimisha siku ya usafi wa hedhi, bado wasichana na wanawake wengi wako na changamoto ya kupata sodo wakati wa hedhi hivyo kufanya usafi wakati huo kuwa vigumu.

Katika kaunti ya Turkana wanafunzi wengi wa kike mara kwa mara hukosa kuenda shuleni kwa sababu ya kukosa sodo wakiwa na hedhi.

Sylvia ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Nameyana.

"Kama niko na sodo, nakuja shuleni lakini kama sina nabaki nyumbani "

Ni taswira ambayo walimu wanaifahamu kwa sababu ni hali halisia kwa wasichsna kukosa kuenda shuleni kwa kipindi fulano kila mwezi.

Image caption Wasichana wa Turkana hupata taabu wakati wa hedhi hulazimika kukosa masomo

"Huwa ninamuomba mwalimu ruhusa ya kuwa niko na shida fulani nyumbani ambayo napaswa kushughulikia lakini simuelwzei shida yenyewe ni ipi."

Jacinta ni mwanafunzi wa darasa la nane katika shule ya Nameyana. Anatarajiwa kufanya mtihani wake wa kitaifa miezi kadhaa zijazo.

"Ninapopata hedhi, siwezi keti darasani, kwa sababu hakuna sodo. Mimj huenda nyumbani na kutengeneza viraka na kuvaa.

Wengi wa wanafunzi hawa hutegemea msaada kutoka shuleni, na wakati wanapokosa wao huwaomba rafiki zao. Na wazazi wao je?

Hali hii inachangiwa pia na hali ya umasikini na ukosefu wa mafunzo muhimu katika jamii.

Nilichobaini ni kuwa, wengi wa wanawake katika kijiji cha Nameyana hawana elimu kwa hivyo wengi wao hawajui sodo ni nini. Wachache tu waliyo na wanafunzi ndiyo wanajua kwa kuona watoto wao wakitumia

Image caption Wanawake wanapokua kwenye hedhi huchafua nguo zao kisha huzibadili

Hedhi kwa wasichana hawa ni karaha

Kwa wanakijiji wengi, sodo ni msamiati.

Je wanawake hutumia nini?

Kijiji cha Nachukui iko kaskazini mwa kaunti ya Turkana. Kijiji hiki kinapakana na ziwa Turkana.

"Sisi huwa hatutumii chochote wakati wa hedhi. Sisi husokia tu kuna kitu kinaitwa sodo lakini hatujawahi kuiona na hatukifahamu" Akiru Akal mkaazi wa kijiji cha Nachukui aelezea.

Akiru anasema kwamba kwa sababu ya kutotumia chochote, nguo zao huchafuka na wao hulazimika kuziosha kwenye ziwa Turkana kila wakati.

"Kina mama huwa wanachimba shimo na kuketi wakati wa hedhi , lakini sisi vijana huwa hatufanyi hivyo kwa sababu tunaficha uchi wetu."

Upatikanaji wa maji katika kaunti hii ya kaskazini mwa Kenya ni Kitendawili. Mazingira yake ni ya jangwa na jamii hii ni ile ya kuhama hama. Ukosefu wa maji huathiri usafi wakati wa hedhi.

"Kwa sababu hili eneo tunaloishi hakuna mvua na visima vyetu hukauka mara kwa mara, sisi hutumia mafuta ya mbuzi na kondoo kama maji kuosha uchafu wa hedhi."

Hakuna duka linalouza sodo katika kijiji cha Nameyana. Ni vyakula tu vinavyouzwa na mafuta ya taa.

Hedhi kwa wasichana hawa ni karaha

Naibu mwalimu mkuu shule ya msingi ya Nameyana anasema kwamba changamoto kuu ya usafi wakati wa hedhi ni ukosefu wa elimu katika jamii

" Wazazi wa watoto wetu wengi hawajawahi kuenda shule, kwa hivyo hata ukimuelezea kuna kitu kinaitwa sodo... hawezi kubali kwa sababu hajawahi labda kuiona na kwa hivyo anashangaa mtu anawezaje kuvaa makaratasi"

Bw Merinyang anasema pia umasikini umechangia na unasababisha kuathirika kwa masomo ya wasichana kwa kukosa shule wakati wa hedhi.

Kwanini visodo vilivyotumika vinakusanywa India?

" Kwa sababu ya njaa, unapata ni vigumu sana mzazi kununua sodo. Wao huchagua kununua unga badala ya kununua sodo ambayo itawaacha wengi na njaa"

Hata hivyo anasema kwamba wamekuwa wakipokea msaada kutoka kwa serikali lakini ni kidogo.

"Msaada wa sodo hatupati kila mara, sisi hupata tu wakati tumetuma maombi na pia hatupati kila siku. Na wakati mwingine huwa tunaambiwa hazipo"

Mada zinazohusiana