Ukomo wa hedhi una athari gani mwilini na utawezaje kukabiliana nazo?

Sura za wanawake Haki miliki ya picha Getty Images

Ukomo wa hedhi ni wakati ambao mzunguko wa hedhi huisha na kwa hali hiyo mwanamke hawezi tena kushika mimba-lakini ni vitu gani hutokea kwa mwanamke huyu wakati wa ukomo wa hedhi na kwa nini?

Ukomo wa hedhi kwa kitaalamu Menopause, ni dalili kuwa umri wa mwanamke umekua mkubwa, hali hii hujitokeza kwa wanawake wenye umri wa kati ya miaka 45 na 55, lakini pia hali hii huweza kusababishwa na upasuaji kuondoa ovari au kizazi (hysterectomy).

Nchini Uingereza wastani wa umri wa ukomo wa hedhi ni miaka 51.

Mabadiliko haya huletwa na nini?

Vichocheo, hususan kichocheo kimoja kiitwacho oestrogen.

Ni muhimu katika mzunguko mzima wa mwezi-uzalishaji wa yai kutoka kwenye ovari kila mwezi kwa ajili ya kurutubishwa.

Lakini wakati wanawake umri wao na na uwezo wa kuhifadhi mayai, ukipungua, hedhi na uwezo wa kushika mimba hukoma.

Na mwili nao huacha kuzalisha kichocheo cha oestrogen, ambacho hudhibiti mchakato wote.

Hata hivyo, hali hii haijitokezi mara moja.Huchukua miaka kadhaa kwa kichocheo hiki kupoteza uwezo wake.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wakati ovari zinazalisha mayai machache wakati umri wa wanawake ukisogea, oestrogen kiasi kidogo huzalishwa mwilini

Madhara gani hujitokeza kutokana na mabadiliko ya kichocheo? (hormone)

Mabadiliko makubwa

Ubongo, ngozi, misuli na hisia huathiriwa kutokana na mabadiliko ya kichocheo cha oestrogen.

Mwili huwa na mabadiliko na wanawake wengi hupata dalili kabla ya kukoma kwa hedhi.

Mwili kupata joto, kutoka jasho wakati wa usiku, wasiwasi, kutokua na hamu ya kujamiiana ni miongoni mwa yanayowakabili wanawake katika kipindi hiki.

Matatizo kwenye kibofu na ukavu kwenye sehemu za uke ni miongoni mwa changamoto.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mifupa huwa dhaifu baada ya kukoma kwa hedhi

Wakati oestrogen inapokoma kuzalishwa, madhara ya muda mrefu hujitokeza kenye mifupa na moyo.

Mifupa inaweza kuwa dhaifu, kiasi cha kuwa na uwezekano wa kuvunjika na wanawake wanaweza kuwa kwenye hatari ya kupata maradhi ya moyo na kiharusi.

Hii ni sababu wanawake hufanya upasuaji ili kukipa nguvu kichocheo cha oestrogen (HRT ) ili kupunguza masumbufu hayo.

Lakini si wanawake wote wanaopitia dalili hizi.Hutegemea ni kwa muda gani dalili hizo hujitokeza kuanzia miezi michache mpaka miaka.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Upungufu wa oestrogen kabla na baada ya ukomo wa hedhi huathiri ubongo na mwili kwa namna nyingi

Oestrogen inaathiri hisia pia?

Ndio, inaweza kuwa hivyo.

Pia upungufu wa oestrogen unaweza kuathiri ngozi, inamfanya mwanamke ahisi ngozi ni kavu na kuhisi kama wadudu wanatembea ndani ya ngozi

Je, kuna vichocheo vingine vinavyohusika?

Ndio, progesterone na testosterone-lakini hazina athari sawa na oestrogen.

Progesterone husaidia kuutayarisha mwili tayari kwa kushika ujauzito kila mwezi, na hufa mara hedhi inapokoma.

Testosterone,ambazo huzalishwa kwa kiasi kidogo na wanawake, huhusishwa na hamu ya tendo la kujamiiana na nguvu.

kichocheo hiki hufa pale mwanamke anapofika miaka ya 30 na zaidi.

Utafiti: baadhi ya vyakula husababisha ukomo wa hedhi mapema

Maajabu ya binti aliyejifungua bila kujua ana ujauzito

Unajuaje kama una dalili za ukomo wa hedhi ?

Ni kwa namna gani utafahamu kama una dalili za ukomo wa hedhi?

Inawezekana kufanya kipimo cha damu kupima kiasi cha kichocheo kipimo kiitwacho FSH (follicle-stimulating hormones) lakini kipimo hicho hakina majibu ya uhakika hasa kwa wale walio na umri wa zaidi ya miaka 45.

Wataalamu wanasema vichocheo hubadilika badilika,nyakati zote hivyo kipimo hicho hakiwezi kutoa majibu ya uhakika kuhusu kinachoendelea.

Namna nzuri ni kuzungumza na mtaalamu kuhusu mwenendo wa hedhi na dalili unazoziona.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption mwili kuwa na joto ni moja kati ya dalili

Kiwango cha oestrogen ndani ya mwili haiwezi kurejea katika hali yake baada ya ukomo wa hedhi.

Wanawake sasa wanaishi zaidi ya robo tatu ya maisha yao wakiwa na kiwango kidogo cha oestrogen.

Laini mtaalamu wa magonjwa ya wakina mama nchini Uingereza Dokta Heather Currie anasema ''pamoja na changamoto zao, wanawake wameendelea kufurahia maisha-sasa mtazamo wa zamani kuhusu kukoma kwa hedhi umebadilika.''

Haki miliki ya picha Getty Images

Mtaalamu huyu anasema kuwa kuna namna nyingi na taarifa nyingi za kusaidia wanawake wakaweza kuishi na mabadiliko ya kimwili na kihisia yanayosababishwa na ukomo wa hedhi.

Tiba ya kuweka vichocheo mbadala ni tiba nzuri inayoweza kupatikana kuondokana na dalili za ukomo wa hedhi.

Na ukomo wa hedhi ni sababu moja wapo kuwafanya wanawake waishi maisha mazuri ya afya kwa:

  • Kula chakula bora, kuepuka mafuta na kula chakula chenye madini ya chuma ili kuimarisha mifupa na kuzuia maradhi ya moyo.
  • Kufanya mazoezi, ili kupunguza hali ya wasiwasi, msongo wa mawazo na kuepuka maradhi ya moyo.
  • Kuacha kuvuta sigara na kunywa pombe kupita kiasi.

Mada zinazohusiana