Kutana na chura anayetambua ujauzito

Chura aina ya Xenopus Laevis Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hii ilikuwa ni sura ya vipimo vya mimba baina ya miaka ya 1930 hadi miaka ya 1970

Chura huyo huyu wa Kiafrika aliishi kwa maisha ya amani katika maji tulivu ya kusini mwa jangwa la sahara kwa miaka mamilioni . Hadi katika miaka ya 1930, mwanasayansi wa Kiingereza alipoamua kumdunga sindano ya mkojo, na hapo ndio ikawa mwisho wake.

Lancelot Hogben alikuw ani mtaalamu wa viumbe wa majini aliyekuwa akiwadunga wanyama kwa kemikali mbali mbali, nyingi zikiwa ni za homoni, lengo lake ni kuangalia matokeo yake yatakuwa ni yapi kwa wanyama.

Baada ya kufanya moja ya vipimo hivi vya uchunguzi, aligundua bila kukusudia kwamba homoni za ujauzito zinaweza kusababisha kutungwa kwa mayai miongoni mwa wanyama hawa.

Haki miliki ya picha Novartis AG
Image caption Vipimo viligundulika kuwa vilikuwa sahihi kabisa kiasi kwamba kwa miongo miwili iliyofuatia, maelfu ya vyura walidungwa sindano za mkojo wa binadamu

Maureen Symons anakumbuka alipopata matokeo ya ujauzito wake baada ya kupimwa kwa kutumia chura aina ya Xenopus katika miaka ya -1960 .

"Nina picha akilini, nilipimwa walau mara mbili , daktari aliyekuwa amevalia koti jeupe akija kuniambaia akiwa ameridhika , 'una ujauzito - chura ametotoa mayai ',"aliiambia BBC.

Haki miliki ya picha Novartis AG
Image caption Kipimo kilikuwa rahisi : Kudunga mkojo ambao haukuchanganywa na kitu chochote chini ya ngozi ya chura jike aina ya Xenopus, halafu unasubiri baada ya saa 5 hadi 12 , na kama ni mjamzito atakuwa ametaga mayai kwa kipindi hicho

Vipimo vya chura aina ya Xenopus havikuwa vinapatikana kwa umma. Vilikuwa vinatunzwa kwa ajili ya matumizi ya dharura, ya kimatibabu - kwa mfano, kutofautisha ukuaji wa ya kijusi na ukuaji wa uvimbe.

Mimba mbili za Maureen zilikuwa zimetoka, na ni vyura tu walioweza kueleza ukweli.

"Nimegundua sasa kuwa nilikuwa na bahati kufanyiwa vipimo vyote hivi ," anasema

Image caption Kutokana na umaarufu wake, kulikuwa na vituo maalum vya upimaji wa kutumia vipimo vya vyura aina ya Xenopus

Mwanahistoria wa masuala ya tiba Jesse Olszynko-Gryn wa chuo kikuu cha Strathclyde anasema ingawa wazo lenyewe linaonekana kuwa si la kawaida maskioni mwa watu wa kizazi hiki cha kisasa , kanuni za kimsingi za kipimo ni sawa tu na zile za kipimo cha nyumbani kwa sasa . Kile hasa kilichobadilika vi vile tunavyozungumzia ujauzito.

"Hebu rejea katika miaka ya 1930 na wakati huo ujauzito ulikuwa ni jambo ambalo halikuzungumziwa . Usingeweza kuchapisha neno 'ujauzito ' kwenye gazeti. Lilikuwa ni neno la kibaiolojia sana na lilionekana ni neno ambalo haikuwa la staha."

Alikuri kuwa kipimo hicho kiliweza kusaidia kuelezea jauzito.

Haki miliki ya picha BBC Ideas
Image caption Vipimo vya kisasa vya ujausito havikuweza kuutambua ujauzito hadi ilipofika miaka ya 1990

" Upimaji wa ujauzito ni ubunifu wa utamaduni mpya katika jamii tunazoishi kwa leo ambao kusema ukweli umeweka wazi suala la ujauzito na uzazi pamoja na elimu ya uzali kwa ujumla ."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii