Je wajua pesa chafu na simu za mkoni ni hatari kwa afya yako?

Kutofuatwa kwa kanuni ya kuosha mikono na usafi kwa ujumla kunasababisha kuhamishwa kwa vimelea hawa wa magonjwa kwenye chakula, umebaini utafiti
Image caption Kutofuatwa kwa kanuni ya kuosha mikono na usafi kwa ujumla kunasababisha kuhamishwa kwa vimelea hawa wa magonjwa kwenye chakula, umebaini utafiti

Pesa chafu na simu za mkononi zinaweza kuwa hatari kubwa kwa afya yako, watafiti wameonya.

Pesa hususani zile za thamani ndogo, wanasayansi wanasema zinasababisha magonjwa mengi ya kuhara, miongoni mwa watu wanatumia chakula kinachoandaliwa kwenye maeneo ya hoteli, migahawa na vilabu.

Wanaoandaa chakula.

Utafiti uliofanywa miongoni mwa waandaaji wa chakula 395 katika maeneo 15 tofauti ya jiji la Nairobi na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Jomo Kenyatta na kile cha teknolojia nchini humo (JKUAT), kwa ushirikiano na taasisi ya utafiti wa masuala ya tiba ya Kenya (Kemri), na Kitengo cha Utafiti wa matibabu cha jeshi la Marekani Kenya.

Image caption Wanaoshughulikia chakula na umma kwa ujumla wanapaswa kuhamasishwa juu ya hatari zinazoweza kutokana na kugawa chakula baada ya kushika pesa au simu za mkononi

Utafiti huo ulionyesha kwamba kwasababu huwa pesa na simu za mkononi huwa hazisafishwi hugeuka kuwa maficho ya vimelea wa magonjwa ambao husababisha sumu kwenye vyakula.

Baada ya kupima sarafu kuanzia shilingi 1 hadi noti ya shilingi 1,000 zinazotumiwa jijini Nairobi, ripoti ilifuchua kuwa sarafu za shilingi 5, 10, 20 ndizo zilizokuwa chafu zaidi zikifuatiwa na noti za shilingi 50, 100 na 200.

"Nyingi kati ya pesa pamoja na simu zilikuwa na bakteria wanaosababisha magonjwa ," matokeo ya utafiti huo yaliwasilishwa kwenye mkutano wa 7 wa Afya na Sayansi wa Afrika Mashariki uliofanyika Dar es Salaam, Tanzania,mwezi Machi.

Baya zaidi bado ni kuwahusu wahudumu wa vyakula, hususan wanaogawa vyakula kwa wateja pamoja na wapishi ambao ilibainika kuwa hawazingatii usafi hasa baada ya kupokea simu zao za mkononi.

Haki miliki ya picha Getty Images

Wakati wa utafiti huo , washiriki 34 walipatikana na magonjwa kama vile kikohozi, kichomi na maumivu ya tumbo na utumbo (gastroenteritis).

Magonjwa haya sababishi matatizo tu kwa wagonjwa, bali ni magonjwa yanayoweza kuambikizwa kutoka kwa muandaaji wa chakula, anayegawa chakula au mpishi wa chakula anayeumwa.

Aidha ilibainika kuwa 60% ya waliofanyiwa utafiti hawa kuwa wamenawa mikono yao baada ya kupokea simu za mkononi .

Kwa kawaida, waandaaji wa chakula hawapaswi kupokea simu.

"Wanaoshughulikia chakula na umma kwa ujumla hawanabudi kuhamasishwa juu ya hatari zinazoweza kutokana na kugawa chakula baada ya kushika pesa au simu za mkononi ," Ulionya utafiti.

Maambukizi ya ngozi

Mnamo mwaka 2009, Taasisi ya utafiti wa tiba nchini Jenya (kemri) ilifanya utafiti sawa na huo jijini na ikagudua kuwa simu za mkononi zina vimelea wa magonjwa kwa kiasi kikubwa baadhi zikiwa hata va vimelea wanaopatikana kwenye kinyeshi .

Nyingi kati ya pesa zilizopatikana na vimelea zilikuwa ni sarafu zilizochukuliwa kutoka kwenye machinjio , zikifuatiwa na zile zilizokusanywa kutoka kwa wauzaji wa mahindi kando ya barabara na vyakula vinavyouzwa kwneye maduka madogo(vioski)

Kwa mujibu wa Daktari Richard Korir, afisa wa utafiti katika kituo cha kitengo cha Utafiti wa Mikrobiologia na muandishi wa utafiti huo, kutofuatwa kwa kanuni ya kuosha mikono na usafi kwa ujumla kunasababisha kuhamishwa kwa vimelea hawa wa magonjwa kwenye chakula ambacho bila shaka kinaliwa.

Utafiti huo ulifanywa na kuwasilishwa mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika Chuo kikuu cha Kilimo JKUAT amabye aliangazia aina mbalimbali za bakteria wanapatikana katika mazingira, chakula, utumbo na ngozi katika wanyama na binadamu.

Simu za mkononi zilikuwa na maambukizi zaidi

Ingawa vimelea vingi vya bakteria hawa si hatari, baadhi wanaweza kusababisha magonjwa kama vile homa ya matumbo, sumu ya chakula na maambukizi ya ngozi.

"Shilingi 1,000 ndiyo yenye maambukizi ya chini kwasababu hutumiwa mara chache, huku sarafu ya shiringi 1 ikiwa pia haina uchafu mwingi na thamani yake imeshuka kwa hiyo haitumiwi sana ," alibaini Daktari Korir.

Haki miliki ya picha KENYA CENTRAL BANK
Image caption Sarafu zenye thamani ya chini ndizo zilizopatikana nauchafu mwingi kuliko zile zenye thamani ya juu

Vimelea waliopatikana zaidi walikuwa ni wa jamii ya staphylococcus, wanaofahamika kusababisha maambukizi ya ngozi, moyo na mifupa , sumu ya chakula, kichomi na sumu ya mwili wa binadamu.

Bakteria waliopatikana katika chakula pia ni jamii ya Escherichia coli (E. coli), ambao hupatikana katika mazingira, chakula, na utumbo wa binadamu na wanyama.

Wengi kati ya vimelea hao si hatari lakini wanaweza kukufanya uwe mgonjwa.

La kushangaza ni kwamba , Daktari Korir alisema, zikilinganishwa na simu za pesa, simu za mkononi ndi mbaya zaidi inapokuja katika suala la maambukizi ya magonjwa.

" Watu wengi hawadhani kuwa simu ni chafu au ni chanzo cha kuambukizwa magonjwa , kwa hiyo , mara nyingi hawazingatii usafi baada ya kuzitumia ," alisema.

Simu ziligundulika kuwa bakteria 12 baada ya kukusanywa na kuchunguzwa na zaidi bakteria aina ya Staphylococcus, ambao mara nyingi hupatikana katika nywele na ngozi.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Teknolojia inavyosaidia kukabiliana na uhaba wa chakula Nigeria

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii