Homoni za kutunisha mwili hatari kwa uzazi wa wanaume

Wanasayansi wanasema inasababisha matatizo makubwa miongoni mwa wanandoa wanaojaribu kupata ujauzito. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanasayansi wanasema inasababisha matatizo makubwa miongoni mwa wanandoa wanaojaribu kupata ujauzito.

Wanasayansi wamefanya mageuzi ya kitendawili kuwa wanaume wanaharibu uwezo wao wa kubapa watoto wakati wanapofanya jitihada za kuwafanya wawe na muonekano wenye mvuto zaidi.

Kutumia kemikali za homoni zinazotumiwa kuongeza maumbile ya mwili (steroids) au tembe za kuzuwia upara ili wawe na nywele kichwa kizima ni mambo yanayoweza kuzuwia uwezo wa uzazi kwa mwanamume.

Mapinduzi ya kitendawili hiki yameitwa Mossman-Pacey - majina ya wanasayansi walioyaelezea.

Wanasema inasababisha matatizo makubwa miongoni mwa wanandoa wanaojaribu kupata ujauzito.

"Niligundua baadhi ya wanaume wakija kwenye kliniki kufanyiwa vipimo vya uzazi na watu hawa walikuwa wana maumbo makubwa ," anasema Dkt. James Mossman, ambaye kwa sasa yuko katika Chuo Kikuu cha Brown University nchini Marekani.

Alikuwa anasomea shahada ya udaktari katika Sheffield alipozungumzia matumizi mabaya ya homoni za kuongeza maumbo ya mwili -steroid

Aliiambia BBC kuwa : "Wanajaribu kuonekana wenye umbo kubwa sana ,kuonekana kama mihimili mageuzi.

" Lakini wanajifanya kuwa watu wasiofaa kabisa katika mageuzi kusema ukweli, kwasababu hali hiyo inawafanya kutokuwa kabisa kutotoa kabisa mbegu za uzazi wanapomalizia tendo la ndoa ."

Image caption Dkt. Mossman na Profesa Pacey: Waanzilishi wa dhana kwamba ya homoni za kuongeza maumbile ya mwili zainawweza kutumiwa kuimarisha nguvu za kiume

Dkt. Mossman na Profesa Pacey: Waanzilishi wa dhana kwamba: Homoni za kuongeza maumbo ya mwili walisema kuwa athari za homoni za kiume mwilini hutumiwa kama dawa za kuongeza nguvu za kiume na kuongeza ukuaji wa misuli

Hutumiwa mara kwa mara na wanaojenga miili yao.

Profesa Allan Pacey, kutoka chuo kikuu cha Sheffield, aliongeza kuwa " Ni kweli kwamba wanaume huenda kwenye maeneo ya mazoezi ya mwili (gym) ili wawe na muonekano wenye mvuto , kwa sehemu kubwa hutaka kuwavutia wanawake na kinyume chake wanapunguza uwezo wao wa kutungisha mimba''.

Homoni za steroids huupumbaza ubongo na kuufanya uhisi kuwa utengenezwaji wa mbegu za uzazi za kiume unapita kiwango.

Hivyo basi kiwango cha utengezaji wa mbegu za kiume hupunga kutokana na kutengenezwa kwa aina mbili za homoni zinazoitwa - FSH na LH -ambazo ni homoni muhimu zinazowezesha uzalishaji wa mbegu za kiume.

Watafiti wanasema kuna baadhi ya wanaume wanaotumia mbinu hiyo ya tiba kujiepusha na tatizo la kuwa na upara.

Tiba hiyo hubadilisha mfumo wa homoni ya kiume mwilini ili kudhibiti hali ya nywele kunyonyoka kinchani lakini huenda akiathiri kizazi cha mtumiaji wa tiba hiyo.

Prof Pacey aliiambia BBC: "nathibitisha kuwa watumiaji wa tiba ya ''anabolic steroid'' huenda wakapoteza kabisa nguvu ya kizazi kwa karibu - 90% .

"Kwa wale wanaotumia kuzuia upara matokeo yako juu kwasababu ni tatizo ambalo linawakabili."

'kupitisha geni'

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanasayansi wanasema mazoea ya kutumia homoni yatakufanya uvutie lakini matokeo yake ni madhara yatakayokupata ''siku zijazo.''

Kigezo cha ufanisi kinapimwa kwa misingi ya jinsi geni inavyopasishwa(mpangilio katika DNA ya mtu binafsi) kutoka kizazi kimoja hadi kingine .

Dr Mossman amesema mazoea ya kutumia dawa hii itakufanya uvuvutie lakini matokeo yake ni madhara yatakayokupata ''siku zijazo.''

Ni sawa na manyoya ya tausi ambayo yanawafanya wanaume kuvutia zadi ya wanawake hali ambayo inaongeza uwezekano wa kupitisha geni hizo kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Kuna baadhi ya mifano katika ulimwengu halisia ambapo wanyama wako tayari kupoteza uwezo wao wa kuzaa ili mradi wadumishe muenekano wao mzuri.

Huwezi kusikiliza tena
Wanaume wafungwa uzazi kwa pamoja Kenya

Baadhi ya ndege hushirikiana kudumisha kizazi katika hali ambapo wengine yao wako radhi kuepuka uzazi ili wasaidie kulei kizazi cha jamaa zao.

Dr Mossman anahofu kuwa "mtu huenda akafikiria anapendeza kwa watu wa jinsia tofauti, lakini wanaua kizazi chao".

Prof Pacey pia ameiambia BBC: "Kinaya ni kitu kimoja, lakini nadhani ujumbe muhimu ni kwa wagonjwa wenye tatizo la kizazi.

"Hili ni tatizo linalojitokeza katika baadhi ya kliniki lakini ujumbe huu hauwafikii vijana ambao wanatumia tiba hii lakini ujube huo ungesaidia."

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Mambo matano kuhusu jinsi wanaume wanavyoathiriwa na fistula

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii