Wafungwa wa Brazil wanabuni mitindo ya mavazi ndani ya gereza

Mfungwa akishona kama sehemu ya mradi wa "Ponto Firme" katika jela la Adriano Marrey la Guarulhos, Brazil Mei 22, 2019. Haki miliki ya picha AFP

Maeneo ya mavazi ya kupendeza na majina makubwa ya wanamitindo ndivyo vinavyotuniwa na wanamitindo katika Wiki ya fasheni ya São Paulo , lakini Jumatano Wednesday badala yake walionyesha ubunifu wa wabunifu wa mitindo ambao hawafahamiki katika eneo ambalo watu wasingependa kushiriki- nalo Gereza kuu la Adriano Marrey.

Mwanamitindo akionyesha vazi la kushonwa kwa uzi lililobuniwa na kushonwa na mfungwa kama sehemu ya mradi wa "Ponto Firme" katika gereza la Adriano Marrey maximum mjini Guarulhos, Brazil tarehe Maei 22, 2019. Haki miliki ya picha AFP

Uwanja wa gereza badala ulitumiwa kama jukwaa la maonyesho ya mavazi yenye rangi za kuvutia yaliyoshonwa na wafungwa.

Wanamitindo wanaojivunia kazi yao na wabunifu wa nguo walifurika kando ya kuta za gereza kushuhudia kwa shauku kazi ya kila mmoja wao . baadhi yao walikuwa ndio bado wanamalizia kazi zao za ubunifu wao wa mavazi ya kisasa.

Mwanamitindo mfungwa akionyesha vazi lake alilolibuni katika jela la Adriano Marrey lililopo Guarulhos, Brazi - May 22, 2019 Haki miliki ya picha AFP

Kwa wabunifu ambao walivalia suruari za kaki na fulana nyeupe, nguo zao zilikuwa za kipekee na zilikuwa na rangi tofauti na kuta za gereza ambazo ni za rangi ya kijivu.

Models present crochet clothing creations made by inmates as part of "Ponto Firme" project in the Adriano Marrey maximum security penitentiary in Guarulhos, Brazil on May 22, 2019. Haki miliki ya picha AFP

Onyesho hili lisilo la kawaida ni sehemu mradi wa kuwarekebisha wafungwa kwa kuwafundisha ushonaji wa nguo

Mradi huo umekuwa ukiendeshwa kwa miaka mitatu na ulibuniwa na mwanamitindo wa Brazil Gustavo Silvestre.

Mbunifu wa mitindo wa Brazil Gustavo Silvestre alipigwa picha kabla ya kuwasilisha mradi wa "Ponto Firme" katika gereza la Adriano mjini Guarulhos, Brazil- Mei 22, 2019. Haki miliki ya picha AFP

Wafungwa wanaojiunga na mpango huo wanapunguziwa vifungo vyao kwa siku moja kila baada ya saa 12 ya kukamilisha kozi yao.

Mfungwa akishona vazi Haki miliki ya picha AFP

Baadhi ya wafungwa wanahudumu vifungo gerezani baada ya kupatikana na makosa kama vile ya ulanguzi wa dawa za kulevya na wizi wa kimabavu.

Mmoja wao Felipe Santos da Silva aliliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa kushona nguo kutokana na uzi wa sweta kunamfanya "atulie, pia ilimsaida kuachana na uraibu wa kuvuta sigara na kutumia mihadarati".

An inmate poses with a crochet clothing creation as part of "Ponto Firme" project in the Adriano Marrey maximum security penitentiary in Guarulhos, Brazil on May 22, 2019 Haki miliki ya picha AFP

Mfungwa mwingineFidelison Borges, 41 alisema hafla hiyo ilimsaidia kupata uwezo wa kujiamini.

"Nilijivunia kuona watu wakitumia mapambo yangu wakati wa hafla hiyo na cha kujivunia zaidi ni jinsi baadhi ya watu walivyopendezwa na mapambo hayo," alisema mfungwa huyo t.

Picha zote zina hati miliki.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii