Wasichana watumia vikopo vya hedhi kujisitiri
Huwezi kusikiliza tena

Wasichana Malawi wanatumia vikopo vya hedhi kujisitiri

Wakati dunia inapoadhimisha siku ya usafi wa hedhi, bado wasichana na wanawake wengi wanakabiliwa na changamoto ya kupata sodo wakati wa hedhi hivyo kufanya usafi wakati huo kuwa vigumu.

Baadhi ya wasichana hawana uwezo wa kununua taulo za hedhi au visodo wakati wanapokuwa kwenye ada yao ya mwezi. Wengine wao wanalazimika kukosa masomo kwa siku kadhaa.

Lakini sasa, wasichana nchini Malawi wanatumia vikopo ambavyo vinawasaidia kujisitiri wakiwa na hedhi. Vikopo hivyo ambavyo vilivumvuliwa kutoka miaka ya 1930 vimeleta mabadiliko makubwa kwasichana kutoka jamii masikini.

Mada zinazohusiana