KPMG: Real Madrid 'ndio timu ghali zaidi barani Ulaya'

Real Madrid v Manchester United Haki miliki ya picha Rob Foldy/Getty

Real Madrid imeipiku klabu ya Manchester United kwa kutajwa kuwa klabu yenye thamani zaidi kibiashara barani Ulaya kwa kiwango cha euro zipatazo bilioni 3.22 kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na KPMG.

Klabu hiyo ya Hispania imetajwa kuwa juu katika thamani ya kibiashara baada ya kuripotiwa kwa matokeo ya utafiti uliofanyika katika msimu wa mwaka 2016 -2017 na 2017-2018 ukiangalia namna timu zinavyopata faida, umaarufu wa timu, umeangalia wa kucheza na thamani ya kiwanja.

Michuano ya mwisho ya ligi ya mabingwa iliiweka Liverpool na Spurs katika nafasi ya saba na tisa .

Na katika ligi ya mwisho ya Ulaya, Chelsea na Arsenal walitajwa katika nafasi ya sita na nane.

Manchester City iko nafasi ya tano, hii ikiwa inamaanisha kuwa klabu sita za ulaya zimeingia 10 bora.

Real Madrid imeshinda mashindano ya ligi ya mabingwa katika misimu miwili ambayo imeweza kuipa timu hiyo fursa ya kuwa juu katika soko kwa asiliamia 10.

Haki miliki ya picha Reuters

Vilevile klabu ya Celtic imejumuishwa katika orodha ya klabu 32 ambazo ziko juu.

Mwandishi wa michezo wa kimataifa,Andrea Sartori, amesema kwamba kwa ujumla thamani ya sekta ya mpira wa miguu imekuwa kwa asilimia 9 ukilinganisha na miaka iliyopita .

"Kwa ujumla thamani ya kibiashara ya klabu 32 za juu imepelekea ongezeko la asilimia 5 kwa jumla katika tozo za kodi" alisema Andera .

Kwa upande mwingine gharama ya wachezaji imeendelea kukua pia hivyo kupelekea klabu hizo bora kuongezeka kwa pointi 4 mpaka asilimia 63."


Klabu bora 10 za ligi la ulaya katika soko

  • Real Madrid - €3.224bn
  • Manchester United - €3.207bn
  • Bayern Munich - €2.696bn
  • Barcelona - €2.676bn
  • Manchester City - €2.460bn
  • Chelsea - €2.227bn
  • Liverpool - €2.095bn
  • Arsenal - €2.008bn
  • Tottenham - €1.697bn
  • Juventus - €1.548bn

Chanzo cha habari: KPMG


Bwana Sartori aliongeza: "Ligi ya Premia imejithihirishia ushindi mkubwa kwa kuwa na klabu tisa ndani ya klabu bora 32 na kubeba thamani ya asilimia 43 ya soka la ulaya kibiashara ."

West Ham United, Leicester City na Everton ni klabu nyingine tatu za Ulaya ambazo zimeingia katika orodha ya klabu bora 32 ingawa zenyewe hazikufanikiwa kuingia katika orodha ya kumi bora.

Huku Inter Milan ambayo ilichukua nafasi ya 15 imeziacha nafasi tano kuwa klabu ya pili kwa thamani nchini Italia na kuongeza asilimia 41 ya thamani ya soko.

Mwaka huu, klabu 13 ziliongezeka thamani na kuzidi euro bilioni 1, ukilinganisha na mwaka 2018.

Na klabu nane ziliripotiwa kuwa na kiwango cha thamani isiyopungua euro bilioni 2; klabu tano kutoka ligi la Premia Uingereza na klabu mbili zikiwa zimetokea Hispania na moja kutoka Ujerumani.

Pamoja na Celtic kuingia katika orodha ya timu bora 32 kwa mara ya kwanza huku klabu ya Uturuki ya Fenerbahce kutoka.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii