Utekaji bado mwiba kwa rais Buhari

Three men arrested in a crackdown down on kidnapping gangs Haki miliki ya picha Nigeria Police Force
Image caption Washukiwa wa utekaji wakiwa wamebeba silaha wakati walipokamatwa na polisi wiki iliyopita

Sherehe za kuapishwa kwa rais Muhammadu Buhari hazitaondoa changamoto kubwa ya ongezeko la utekaji linalomkabili rais huyo akiwa anaingia awamu ya pili ya utawala wake.

"Vijana nane waliagizwa kutulinda. wakiwa wanavuta sigara na bangi huku wakitukana na kutishia kutuua kwa sababu hawajalipwa kiwango walichokuwa wanakitaka,"

Watekaji nchini humo wamekuwa wanawateka matajiri kwa maskini, na mara nyingi hukusanya kiasi cha dola 150,000 na wengine uwauwa mateka wake pale ambapo familia ikishindwa kutoa kiwango wanachokitaka.

Haki miliki ya picha NIGERIAN ARMY

Mwaka jana kabla ya mashinano ya kombe la dunia, mchezaji wa timu ya Nigeria na Middlesbrough John Mikel Obi alisema kwamba baba yake aliwahi kutekwa mara ya pili na kutishia kumuua.

"Nadhani ilikuwa baada ya mechi ndio niliambiwa kuhusu hilo na walikuwa wanataka kumpiga risasi,"

Aliongeza kusema kuwa walilipa dola 28,000 ili baba yake aweze kuachiwa huru.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Miaka mitano imepita tangu wasichana wa 100 wa Chibok walipopotea

Buhari alipoingia madarakani mwaka 2015, alihaidi kutokomeza kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo limeathiri maisha ya maelfu ya watu kaskazini mashariki mwa nchi ambalo limekuepo kwa miongo.

Wengi walibaki bila makazi na huku wasichana 100 waliotekwa wakiwa shuleni hawajapatikani

Kwa sasa wasiwasi wa kiusalama bado upo katika maeneo ya kaskazini katika maeneo ya Zamfara, Kaduna na Katsina na kuliacha taifa hilo kuathirika na ugaidi .

Kumekuwa na uhaba wa chakula katika taifa hilo na hii ni kutokana na hofu waliyonayo wakulima kuogopa kwenda shambani.

Changamoto zinazomkabili Buhari

Haki miliki ya picha AFP

Usalama: Matukio ya utekaji na mauaji haswa magharibi mwa nchi hiyo yamekuwa yakiendelea licha ya serikali kudai kuwa imelitokomeza kundi la kiislamu la Boko Haram ambalo linahusishwa na kundi la kigaidi la 'Islamic state'

Uchumi: Asilimia 70 ya mapato ya serikali yake yanategemea mafuta, na sasa bei ya mafuta imeshuka na kulifanya taifa hilo kuanguka kiuchumi. Benki ya dunia imekadiria kuwa uchumi umepungua kwa asilimia 2.2 , hali ni mbaya kwenye upande wa ajira ambapo ni zaidi ya asilimia 20 hawajaariwa na karibu nusu ya idadi ya watu wa nchi hiyo ni maskini.

Rushwa: Rais amefanya jitihada katika utawala wake kwa kupambana na rushwa , ambapo zaidi ya dola bilioni kumi ziliweza kurejeshwa katika kodi. Lakini amekuwa akikosolewa kwa kutowachukulia hatua baadhi ya watendaji wake ambao walihusishwa na rushwa. r

Miundombinu: Licha ya mabilioni ya fedha kutumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi , bado hasara iliyotokana na ujenzi huwa inakadiriwa kufika dola bilioni 878 ifikapo mwaka 2040 na hivyo kufanya biashara kuwa na ugumu.

Mwezi uliopita zaidi ya watu 4000 ya wanaigeria na raia wa kigeni walitekwa .Ingawa baadhi ya wabunge waliliona jambo hilo kama changamoto kubwa katika taifa.

Mkuu wa polisi Mohammed Adamu alisema kuwa kati ya mwezi Januari na Aprili mwaka huku watu wapatao 685 walitekwa katika nchi nzima, watu 365 walikuwa wametokea eneo la kaskazini.

Washukiwa 93 wa utekaji walikamatwa wiki mbili zilizopita.

Rais Buhari alijibu suala hilo la utekaji kupitia mitandao ya kijamii, " Nadhani anapungua uzito hivyo nadhani anafanya kazi sana"

Mjadala uliibuka katika mtandao wa kijamii na kudai kuwa ni sawa na kumkejeli rais

"Ukosefu wa ajira unasababisha kukua kwa makundi ya vijana kufanya uhalifu," Mchambuzi wa kimataifa wa masuala ya usalama alieleza.

"Rushwa kuendelea kuepo miongoni mwa wanasiasa inaathiri kwa ukubwa maendeleo na kuhamasisha uhalifu kuendelea"


Muhammdu Buhari ni nani?

  • Alizaliwa 1942 katika familia ya Kiislamu katika jimbo la kaskazini la Katsina
  • Akiwa mwanajeshi wa zamani , aliongoza utawala wa kijeshi wa 1980, anakumbukwa kwa ukali wake kwa wafanyikazi wazembe wa serikali ambao walilazimika kuruka kama vyura hadharani.
  • Alishinda uchaguzi wa urais wa 2015 , akiwa mgombea wa kwanza wa upinzani kufanikiwa kumshinda rais aliyepo madarakani baada ya kuahidi kukabiliana na Boko haram na kumaliza ufisadi.
  • Alimwambia mkewe kwamba anafaa kuwa jikoni baada ya kulalamika kuhusu mahojiano na BBC
  • Baada ya kutoweka kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa alilazimika kukana uvumi kwamba mahala pake palikuchukiliwa na mtu anayefanana naye.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii