Je, kurejeleza taka kuwa bidhaa kutaokoa Ulimwengu?

Paper at a Chinese recycling plant Haki miliki ya picha Getty Images

Ni kampuni inayomilikiwa na mwanamke shupavu, ina mafanikio makubwa huko Hong Kong na Marekani, lakini malighafi yake kuu ni takataka.

Katika mji wa viwanda wa Donggun, Hong Kong kuna kiwanda cha karatasi ambacho ni kikubwa zaidi duniani chenye ukubwa ulio sawa na viwanja 300 vya mpira.

'Nine Dragons' ni kiwanda cha kurejeleza bidhaa kutoka kwenye taka kinachomilikiwa na Bi Zhang Yin, ambaye anajulikana pia kama Cheung Yan, ambaye aliwahi kuandikwa katika jarida la Forbes kuwa ndio mwanamke tajiri zaidi duniani.

Bidhaa zinazotengenezwa katika kiwanda hicho husafirishwa zaidi China na Marekani.

Ingawa si kazi rahisi kuweza kupata karatasi hizo chafu zikiwa katika kiwango kinachohitajika kwa sababu kama baadhi zimeathirika na sumu basi shughuli hiyo haiwezi kufanikiwa.

Nguvu kazi ya binadamu ndio inayohitajika zaidi .

Kwa sasa nchi tajiri zimeanza kuagiza takataka kutoka nchi maskini ambazo wafanyakazi wake wanaoweza kutenganisha taka kwa gharama nafuu ili faida iweze kupatikana.Tangu mwaka 1980 mpaka miaka ya hivi karibuni, mfumo huu umeanza kufanya kazi vizuri.

China ikiwa nchi inayokuwa kiuchumi kwa kasi imeweza kutengeneza bidhaa nyingi.

Waliona bora meli zinazopeleka bidhaa zake katika nchi nyingine kwa mauzo ni vyema kurudi na taka ambazo wanaweza kuzibadili kuwa bidhaa.

Mjasiliamali kama Bi. Yin ameweza kupata utajiri mkubwa kutokana na takataka.

Haki miliki ya picha Getty Images

China ikiwa inazidi kuwa tajiri, serikali yake ilipiga marufuku kwa nchi yake kutokuwa eneo la kutupa taka duniani.

Mwaka 2017, Serikali hiyo ya China iliweka sera ya kukubali taka zinazoweza kutengeneza bidhaa nyingine za mbadala zisizohusisha zaidi ya nusu asilimia ya wafanyakazi wake.

Hayo yalikuwa mabadiliko makubwa ambayo kiliyumbisha biashara hiyo.

Kiwango cha takataka kilichokuwa kinatumwa China kilibadilika ghafla.

Serikali na kampuni za kubadili taka kuwa bidhaa zinajaribu kuendana na mfumo uliopo.

Swali ni Je, wanaweza kupata nchi nyingine ambazo zitakuwa tayari kuokota taka ambazo ni maskini, au kuongeza kodi kwa wafanyakazi wenye mishahara ya juu au kuacha na kuamua kufanya shughuli nyingine ?

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Indonesia ndio nchi ambayo inapokea takataka za plastiki zaidi tangu China ilipopiga marufuku

Kuna sababu ya kupunguza taka, kuzitumia tena na kutengeneza bidhaa mpya kwa mpangilo.

Kuosha chupa na kuzitumia tena kunaleta maana zaidi ya kuzichakata na kutengeneza bidhaa mpya.

Mfumo wa kurudia kutumia bidhaa ulianza kabla ya karatasi hazijaanza kutengenezwa kwa mara nyingine baada ya matumizi, ambayo hii ikiwa inamaanisha kuwa ni sawa na kusafisha na kutumia tena .

Miaka 1000 iliyopita , Japan ilikuwa inatengeneza karatasi zilizotumika kwa kutengeneza karatasi nyingi zaidi.

Kwa miongo watu wamekuwa wakikusanya bidhaa zisizotumika na kuziuza katika viwanda vya karatasi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wakusanyaji taka mjini Paris mwaka 1913

Lakini soko ndio lilikuwa linaelekeza rasilimali ambazo zilikuwa zinahitajika.

Wazo lilikuwa ni kubadilisha taka hizo kutumika tena kwa sababu ndio lilikuwa jambo sahihi .

Bidhaa zote ambazo zilikuwa zinatumika mara moja na kutupwa, zilikuwa zikiokotwa.

Haki miliki ya picha The LIFE Picture Collection/Getty Images

Lakini je watu wanaweza kuacha kuharibu mazingira?

Haki miliki ya picha Alamy

Kwa upande wao India, walikuwa wana ujumbe tofauti, watu walikuwa wanawajibika na taka zao wenyewe

Utengenezaji wa bidhaa kutoka taka lilikuwa jukumu la serikali za mtaa

Haki miliki ya picha Getty Images

Mfumo huu wa kuacha jukumu kwa raia lilibaki kuwafanya wengi kuhoji tatizo liko wapi na huku wengine wakiona kuwa halikuwa jambo sahihi kulifanya.

Ili utengenezaji wa bidhaa mbadala wa taka kuonekana kuwa mzuri lazima wahusika wenyewe waelewe.

Shughuli hiyo ilionekana kutowagharimu huku kiuhalisia inawagharimu.

Mchumi Michael Munger pia alihoji kuhusu wazo la kuacha shughuli za kukusanya taka liwe katika soko huru .

Kama watu watashitakiwa kwa kutupa taka hovyo basi wanaweza kutumia njia nyingine ambayo ni kinyume na utaratibu ,jambo ambalo ni baya zaidi.Lakini kama kodi itatozwa katika bidhaa hizo za taka, kuna hatari ya kuwafanya wananchi kushindwa kumudu gharama.

Namna gani tunaweza kutengeneza bidhaa kutokana na taka?

Aliongeza kusema kuwa wanapaswa kulinganisha gharama na faida ya kubadilisha bidhaa za taka kama chupa, vikombe vya plastiki na bidhaa nyingine.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mfumo wa sasa wa kutengeneza umeme kwa kutumia taka ni jambo salama zaidi .

Bidhaa zinazotokana na taka zinaweza kuwa chanzo cha nishati.

Kama kubadilisha bidhaa ni jambo zuri au la, na lini wanapaswa kuacha?

Mpango wa kurejereza taka . unaweza kupangwa kwa urahisi licha ya kuonekana kama jambo lililopita na wakati.

Taiwan iliwahi kuacha kurejereza bidhaa taka lakini sasa ni nchi maarufu kwa kubadilisha kuwa bidhaa duniani

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Taiwan imesifiwa kwa kuweza kufanikiwa kurejereza bidhaa taka kwa asilimia 55

Kama wao wanaweza kubadili taka kuwa bidhaa kwa nini nchi nyingine wasiweze?

au labda teknolojia inaweza kuja kuokoa watu katika shughuli hizi.

Hakuna kinachoweza kufanyika kama shughuli hiyo itafanywa kwa kuwalipa wafanyakazi kiasi kidogo cha fedha lakini pia inawapa watu fursa ya uzinduzi wa mahitaji mbalimbali katika sekta ya uzalishaji.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii