Unaweza kumlipa mwanamke mwingine abebe mimba kwa niaba yako?
Huwezi kusikiliza tena

Mwanamke mmoja alipa dola elfu 20 kumpata mtoto

Bi Joyce Lay ni kiongozi wa kisiasa ambaye ameyapitia mengi katika maisha yake , alitumia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 5 za Kenya kupata mtoto kwa njia ya kisayansi ijulikanayo kwa jina Surrogacy.

Kwa kifupi ilibidi mwanamke mwingine ambebee mimba kwa kuwa yeye hana uwezo wa kushika mimba wala kuibeba.

Anne Ngugi aliketi naye alipoeleza pandashuka za kutafuta mwanae ambaye sasa ana miaka saba.