Marufuku ya plastiki- Ushauri kutoka Zanzibar
Huwezi kusikiliza tena

Marufuku ya plastiki: Ushauri kutoka Zanzibar

Kuanzia Juni 1, 2019 itakuwa ni kosa la jinai kutengeneza, kuagiza, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki nchini Tanzania, na wote watakao kaidi marufuku hiyo watakutana na mkono wa sheria.

Marufuku hiyo inahusisha maeneo yote ya Tanzania Bara. Lakini upande wa pili wa muungano Visiwa vya Zanzibar vimekua vikitekeleza marufuku hiyo kutoka mwaka 2006.

Mwandishi wa BBC Eagan Salla alifika visiwani Zanzibar na kuzungumza na baadhi ya wakaazi ili kufahamu jinsi walivyofikia utekelezaji wa marufuku hiyo na ushauri wao kwa wenzao wa Tanzania Bara.

Mada zinazohusiana