Je wajua kuwa tumbaku ilikua ikitibu maradhi?

Mtafiti Gilles Everaerts Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mtafiti wa masuala ya kitabibu Everard aliamini tumbaku ina nguvu na kuwa ingewasabisha baadhi ya madaktari kushindwa kufanya kazi

Tumbaku huua mpaka nusu ya watumiaji wake, kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO), kila mwaka watu milioni 6 watapoteza maisha kutokana na matumizi ya tumbaku, wakati karibu watu 900,000 wasiotumia watapoteza maisha kutokana na kuvuta hewa yenye moshi wa tumbaku.

Kwa karne nyingi, uvutaji ulionekana kama ni jambo jema lenye afya na mmea wa tumbaku, Nicotiana, ulipewa jina la kubuni la ''mmea mtakatifu'' na ''dawa ya Mungu'' katika karne ya 16.

Mtafiti wa masuala ya kitabibu kutoka Uholanzi Giles Everard aliamini kuwa faida zinazopatikana kwenye Nicotiana zitafanya kuwe na uhitaji mdogo wa matabibu.

''Moshi mdogo sana wa tumbaku yaweza kuwa dawa dhidi ya sumu aina zote ,'' aliandika kwenye kitabu chake mwaka 1587 kiitwacho panacea: au Universal Medicine, being a Discovery of the Wonderful Virtues of Tobacco taken in a pipe.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tumbaku nyingi asili yake Amerika, zilitumika kama dawa kabla ya kuwasili wazungu karika karne ya 15

Mwanasayansi wa kwanza wa kiingereza kujaribu kutumia tumbaku kwa ajili ya tiba alikua Christopher Columbas, kwa mujibu wa makala iliyoandikwa na Profesa Anne Charlton katika jarida la the Royal Society of Medicine.

Mwaka 1942, aligundua kuwa tumbaku huvutwa kwenye mabomba maeneo ya visiwani kwa sasa kama Cuba, Haiti na Bahama.Wakati mwingine majani huchomwa moto ili kuua vijidudu na kuondoa maradhi na uchovu.

Tumbaku, ilichanganywa na chokaa na limao, na kutumika kama dawa ya meno ambayo ilitumika Venezuela- lakini inaendelea mpaka leo nchini India.

Haki miliki ya picha Wellcome Collection
Image caption Tumbaku ilikua ikitumika kama tiba

Matabibu kutoka Ulaya walivutiwa na matumizi ya dawa zinazotokana na tumbaku.

Katika karne zilizofuata, kwa mujibu wa kumbukumbu ya masuala ya afya, Sigara ikawa lazima kwa daktari, daktari wa upasuaji na wanafunzi wanaosomea udaktari na vyumba vya upasuaji.

Moshi wa tumbaku ulisaidia kukata harufu inayotoka kwa mwili wa mtu aliyekufa na kuzuia maambukizi ya magonjwa yanayotokana na mwili wa mtu aliyekufa.

Wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa tauni jijini London mwaka 1665, watoto walishauriwa kuvuta tumbaku wakiwa darasani.

Haki miliki ya picha Wellcome Collection
Image caption Moshi wa tumbaku ulitumika jijini London mwaka 1665 kupambana na ugonjwa wa tauni

Moshi wa tumbaku uliaminika kuzuia harufu mbaya ambayo iliaminika kubeba magonjwa.

Watu waliokuwa na jukumu la kuzika miili walikua wakivuta tumbaku ili kuepuka maradhi ya tauni.

Pamoja na hayo yote wadadisi wa mambo walihoji kuhusu ufanisi wa tumbaku kama dawa.

Haki miliki ya picha Wellcome Collection
Image caption Katika Karne ya 18, Tumbaku ilitumika kutoa huduma kwa watu waliopata ajali ya kuzama majini

Pamoja na hoja hiyo, bado tumbaku ilikua ikihitajika kwa kiasi kikubwa na wauza dawa walihakikisha kuwa haikosekani .

Moja kati ya matumizi yasiyo ya kawaida ya tumbaku kama dawa ni kumpulizia moshi wa tumbaku mtu aliyenusurika kuzama.

Wataalamu waliamini kuwa moshi humpa joto na kumsisimua mtu mwenye usingizi.Dawa hizi zilipatikana kando ya mto kwa ajili ya hali ya dharura inayoweza kujitokeza.

Kupulizia moshi wa tumbaku sikioni pia ilielezwa kuwa ni dawa kwa maumivu ya sikio katika kipindi cha karne ya 18.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Chapa ngamia iliyokua ikidaiwa kuwa inashauriwa na madaktari kutumika

Baada ya kuondolewa kwa sumu ya nikotini kutoka kwenye majani ya tumbaku mwaka 1828, matabibu duniani wakawa na mashaka na kutoiamini tena tumbaku kama mmea pekee wa tiba.

lakini tiba ya tumbaku iliendelea kupatikana, ikitibu ukosefu wa choo na minyoo.

Uvutaji wa tumbaku ulianza kushika kasi miaka ya 1920 na 1930, kukitengenezwa sigara za chapa ya ngamia zilizokua zikiwahakikishia wateja kuwa madaktari wanashauri uvutaji na uvutaji wa sigara chapa ya ngamia.

Pakiti zilikua na ujumbe kuwa waimbaji wanashauri kuvuta tumbaku ili ''kulisafisha koo''.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tangazo linaeleza kuwa unahitaji kuvuta ilikusafisha koo

Katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, madhara ya uvutaji tumbaku yamekua wazi, hasa kutokana na uvutaji wa muda mrefu.

Hali hii imesababisha nchi nyingi kupiga marufuku uvutaji sigara kwenye maeneo ya wazi.Kampeni zinazotoa elimu zilibeba ujumbe wa kushtua ili kuweza kutimia azma yake kwa Umma.

Aandika historia yake akitahadharisha uvutaji sigara kabla ya kifo chake

Marlboro kuzalisha bangi

Baadhi ya nchi ilikua ni lazima vifungashio vya sigara vibebe ujumbe mzito kwa picha kutahadharisha madhara ya tumbaku kama vile saratani, magonjwa ya moyo na magonjwa mengine yanayosababishwa na tumbaku.

Nchini Uingereza, mwanasesere kwa jina 'Smokey Sue' alikua akitumika kuelemisha wanawake wajawazito hatari ya kuvuta sigara.

Haki miliki ya picha Science Museum London
Image caption Mwanasesere akitoa elimu kwa mama mjamzito

Shirika la afya duniani linasema kuwa tumbaku ni hatari na ni tishio kwa afya ya wanadamu.

Imezitaka nchi kutunga sera kuzuia matumizi ya tumbaku, kama vile kudhibiti matangazo ya sigara , viwanda vya sigara na kuongeza kodi ya bidhaa hizo.

WHO imesema matumizi ya tumbaku yamepungua: asilimia 20 ya watu duniani walivuta tumbaku mwaka 2016 tofauti ya asilimia 27 mwaka 2000, lakini kasi hii si kubwa kiasi cha kufikia malengo yaliyowekwa.

Kuna wavutaji tumbaku bilioni 1.1 watu wazima, asilimia 80 katika nchi zenye uchumi wa kati na nchi zenye uchumi mdogo.