'Mtoto aliyezaliwa akiwa na uzito sawa na tufaha ameondoka hospitalini nchini Marekani

Mtoto mchanga Saybie ameondolewa kutoka hospoitalini Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtoto mchanga Saybie ameondolewa kutoka hospoitalini

Mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa na uzito wa gramu 245 ambaye aliaminiwa kuwa ndiye mtoto mwenye uzito mdogo zaidi wa mwili duniani kuwahi kuzaliwa ameruhusiwa kuondoka hospitalini nchini Marekani.

Saybie alikuwa na uzito sawa na ule wa tufaha kubwa alipozaliwa katika wiki ya 23 ya ujauzito mwezi Disemba mwaka 2018.

Baada ya kuzaliwa alipelekwa kwenye kituo cha tiba ya dharura katika hospitali ya Mary Birch mjini San Diego, California.

Madaktari waliwaambia wazazi wa Saybie kuwa ana saa kadhaa tu za kuishi.

Hata hivyo miezi mitano baadae sasa ameweza kuruhusiwa kuondoka hospitalini akiwa mwenye kila 2.5, akiwa mwenye afya tele,kinyume na matarajio.

Muuguzi ambaye alimuhusumia Saybie alipokuwa aking'ang'ana kuishi alisema kuwa kuishi kwake na kuruhusiwa kwenda nyumbani ni "muujiza ".

taasisi ya usajiri ya watoto wenye mwili mdogo zaidi inadhani Saybie ndiye mtoto kijusi mwenye mwili mdogo zaidi ambaye ameweza kunusurika na kifo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Saybie ameondoka hospitalini baada ya kuwa katika chumba cha matibabu ya dharura kwa miezi mitano

Rekodi ya awali ya mtoto aliyezaliwa akiwa na mwili mdogo zaidi, ilikuwa inashikiliwa na msichana kutoka Ujerumani ambaye alizaliwa akiwa na kilo 252 mnamo mwaka 2015,kwa mujibu wa taasisi ya usajili wa watoto wenye umri mdogo zaidi yenye makao yake katika Chuo Kikuu cha Iowa nchini Marekani.

Mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa na uzito wa gramu 268 nchini Japan mapema mwaka huu anakisiwa kuwa ndiye mvulana aliyeweza kuishi baada ya kuzaliwa kama kijusi chenye uzito mdogo zaidi duniani.

Mama yake Saybie alijifungua kwa njia ya upasuali al maarufu C-section miezi mitatu kabla ya muda wake wa kujifungua haujafika.

Katika video iliyotolewa na hospitali, mama yake alielezea kujifungua kwa mtoto wake kama "siku ya kutisha zaidi katika maisha yake ".

" Nilikuwa kila mara ninawaambia : 'Atanusurika . Ndio -Nina wiki 23 tu za ujauzito ," alisema mama huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Saybie alikuwa na uzito wa gramu 245g na alikuwa na urefu wa sentimita 23 wakati alipozaliwa

Alizaliwa wakati muda wake wa kuzaliwa ukiwa bado kabisa haujatimia madaktari walimchukuliwa kama "kiumbe wa kuchunguzwa kwa kifaa kama cha uchunguzi wa viumbe wadogo sana mithili ya bakteria" . Kwa kawaida mtoto anatakiwa kuzaliwa katika wiki ya 42 ya ujauzito, ilieleza hospitali.

Alikuwa mdogo saana kiasi kwamba mwili wake "uliweza kutosha kwenye kiganja cha muuguzi ", ilisema hospitali.

Chui amjeruhi mtoto mchanga nchini India

Kunusurika kwake na kijfo, madaktari wanaamini, kunatokana na kwamba hakuwa na matatizo makubwa wakati alipozaliwa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii