Mchezaji Filamu wa Hollywood Idris Elba aizuru Tanzania

Elba ni maarufu sana katika umahiri wake wa kucheza filamu za Hollywood na uigizaji wa televisheni

Mchezaji Filamu wa filamu za Hollywood Idris Elba anaizuru Tanzaniana mkewe aliyemuoa hivi karibuni

Bwana Elba ambaye ni maarufu sana katika umahiri wake wa kucheza filamu za Hollywood anaambatana na mkewe ambapo tayari wamekwishazuru mbuga ya wanyama ya Serengeti National mkoani Mara , ambayo ni maarufu sana kwa utalii wa wanyamapori.

Mkewe Elba , Sabrina Dhowre, ametuma picha za wawili hawa katika ukurasa wake wa kijamii wa Instagram ambapo aliwashukuru waongozaji wa matembezi yao kwenye mbuga hiyo.

Wawili hao walifunga pingu za maisha katika sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika mjini Marrakesh nchini Morocco mwezi Aprili 2019 kulingana na jarida la Vague la Uingereza:

Idris Elba mweye umri wa miaka 46 ni drissa Muingereza, mchezaji mzalishaji na muongozaji filamu, mwanamuziki, DJ, na muimbaji wa muziki wa kufoka(rap). Anafahamika zaidi kwa uiogizaji wake katika nafasi mbali mbali za vipindi vya televisheni .

Elba, ambaye ana asili ya Ghana na Sierra Leone aliteuliwa kuw mshindi wa vipindi kama Stringer Bell katika msururu wa HBO ,The Wire, DCI John Luther katika kipindi cha BBC One cha Luther na Nelson Mandela katika historia fupi ya filamu ya Mandela: Long Walk to Freedom (2013).

Aliteuliwa pia mara nne kuwa kwa tuzo ya Golden Globe Award kwa kuwa muigizaji bora wa misururu mifupi ya filamu ambapo alishinda mara moja na aliteuliwa mara tano kuwa mshindi wa Emmy Award.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii