Shule inayotoza karo kupitia taka za plashtiki
Huwezi kusikiliza tena

Shule inayotoza karo kupitia taka za plastiki

Akshar Forum katika Jimbo la Assam Mashariki mwa India imebuni njia ya kipekee ya wanafunzi kulipa karo ya shule. Wanahitajika kupeleka taka za plastiki kila wiki. Mradi huo ulianza kutekelezwa mwezi Oktoba mwaka 2018 baada ya waanzilishi wake kugundua kuwa plastiki zinachomwa nje ya nyumba zao. Kampeni hiyo ya kulinda mazingira ni moja ya miradi inayoendeshwa katika shule hiyo ambapo wanafunzi wanapewa elimu ya kawaida na mafunzo ya ziada itakayowawezesha kujitegemea baada ya kukamilisha masomo yao ya msingi.

Mada zinazohusiana