Mauaji Cameroon: Waliyomuua mwanamke huyu wafichuliwa
Huwezi kusikiliza tena

Mauaji Cameroon: Waliyomuua mwanamke huyu wafichuliwa

Mnamo Julai 2018 kanda ya video inayotisha ilisambaa katika mitandao ya kijamii.

Inawaonyesha wanawake wawili na watoto wawili wakielekezwa huku wakiwa wamehsikiwa bunduki na kundi la wanajeshi wa Cameroon.

Baadae walifungwa macho na kulazimishwa kukaa chini na wanapigwa risasi mara 22.

Serikali ya Cameroon awali ilipuuzilia mbali video hiyo ikidai ni 'habari za uongo.'

Lakini ni nini kilichofuata baada ya taarifa hiyo kuchapishwa?